MWANZA: Viongozi wa kampuni ya ujenzi waliomkacha Waziri Mavunde watakiwa kuripoti Polisi

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Baada ya uongozi wa Kampuni ya Ujenzi ya Jesco ya jijini Mwanza kumkacha ‘kiaina’ Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amewataka viongozi hao kuripoti kwa Kamanda wa Polisi wa Mwanza leo Februari 26, 2018 saa 10 jioni.

pic+mavunde.jpg

Mavunde ametoa kauli hiyo baada ya leo asubuhi kufika katika ofisi za kampuni hiyo eneo Ilemela na kukuta wafanyakazi wa ngazi za chini pekee, huku viongozi wote wakiingia mitini.

Kutokana na viongozi hao ‘kumkimbia’, Mavunde aliamua kuweka kambi kwenye ofisi hizo hadi kieleweke huku akiahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ukiukwaji wote wa sheria na taratibu za kazi.

Licha ya kuwasubiri viongozi hao kwa zaidi ya saa moja hawakutokea na ndipo alipoamua kuondoka eneo hilo na kutaka waripoti kwa kamanda huyo.

Mavunde ametoa agizo hilo baada ya kusubiri viongozi hao ofisini kwao wa zaidi ya saa nzima bila mafanikio.

Pamoja nao, naibu waziri pia ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuwasalimisha kwenye mamlaka husika wafanyakazi wawili raia wa kigeni walioajiriwa kinyume cha sheria.

“Kosa lingine ni kutojisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (CWF), licha wizara kutoa maagizo ya kufanya hivyo mwaka mmoja uliopita,” amesema Mavunde.

Amesema iwapo tuhuma dhidi ya uongozi huo zitathibitishwa, wahusika wanakabiliwa hatari ya kufungo cha miaka sita jela au faini ya Sh50 milioni au adhabu zote kwa pamoja.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii kampuni siwanajenga barabara musoma na kahama, labda walikuwa site, siunajua wabongo kwa kidebe noma, ukitoka kidogo umelizwa, pia jpm yuko chato labda walienda kusaka tenda za chato, utajuaje?
 
Hahaha wajiunge na CWF wakati kazi yao inaisha?! Yani hata day worker nao CWF?! Mtakoma
 
Pale unapolazimishwa kucheka huku unalia moyoni. Hawa Polisi nao wana mioyo jamani. Wasitumike sana. Tunaishi nao huku kitaa. Wana ndugu jamaa,washikaji na marafiki.
 
Back
Top Bottom