Mwanza;ufisadi hadi kwenye makazi ya watu

Mwanza;ufisadi hadi kwenye makazi ya watu

sapt

Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
6
Reaction score
1
picha,za mtaa wa unguja jijini mwanza,hapa ni makazi ya watu,kuna shule za chekechea,msingi(mbugani) na secondari(thaqaafa) na hospital(usumau dispensary),

sheria zinavunjwa wazi wazi,kisha kuna baadhi ya vigogo wa jiji wanapozwa kwa kitu kidogo.huku wakazi wa mtaa na wapita njia wakiambulia hatari kibao,ni hivi majuzi tu mtoto mdogo wa darasa la kwanza amegongwa na gari na kuumia vibaya sana,na siku za hivi karibuni kumewahi kutokea ajari kama hiyo iliyopelekea kupoteza uhai wa mtoto mwingine.

waandishi wa habari jijini wapo kimya,sijui nani wanamuogopa,wananchi wa mtaa husika tumeshawahi kuita wanahabari lakini hawakuweza kutokea.Diwani wa kata ya mbugani,nini majukumu yako kwa wananchi wako?tumewahi kukuita,hali halisi ukaiona,hakuna hatua yoyote uliyochukua,au na wewe wanakupatia rushwa?

Meya wa ccm,chini ya utawala wako,tangu upewe kiti hicho,kwanini sheria zinaendelea kuvunjwa namna hii?
 

Attachments

  • Picture 001.jpg
    Picture 001.jpg
    672.1 KB · Views: 109
  • Picture 002.jpg
    Picture 002.jpg
    646.6 KB · Views: 92
  • Picture 003.jpg
    Picture 003.jpg
    573.4 KB · Views: 71
  • Picture 004.jpg
    Picture 004.jpg
    580.2 KB · Views: 71
  • Picture 005.jpg
    Picture 005.jpg
    545.5 KB · Views: 69
  • Picture 006.jpg
    Picture 006.jpg
    596.5 KB · Views: 69
Ndo madili ya viongozi wetu, hawajali utu bali mali zaidi!! sijui hizo mali ndo zitawazika siku wakifa. Eneo nalijua sana hilo, nimecheza mpira hapo, nimefundisha Thaqafa baada ya kumaliza six, kuna wasomali kibao na madili machafu. Viongozi wetu wangekuwa wako madarakani ili kuwasaidia watu kusingekuwa na matatizo madogo madogo kama hayo. So sad, RIP mtoto.
 
Serikali yenu imeshindwa kuwalinda, kifuatacho ni kujilinda nyie wenyewe; Tafakari chukua hatua kabla ya hatari.
 
Back
Top Bottom