MWANZA: TFDA yateketeza vyakula ,dawa na vipodozi vyenye viambata vya sumu ilemela

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Mamlaka ya chakula na dawa ( TFDA ) kanda ya ziwa, imeteketeza zaidi ya tani 14 za vyakula, dawa na vipodozi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170, vyenye viambato vya sumu na ambavyo vimekwisha muda wake wa matumizi vilivyokamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizoendeshwa na mamlaka hiyo katika Manispaa ya Ilemela na jiji la Mwanza.

Mkaguzi Mwandamizi wa chakula wa TFDA kanda ya ziwa Julius Panga amesema bidhaa zilizoharibiwa kwa kuchomwa moto ni kilo 884 za vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu vyenye thamani ya shilingi milioni 7.5,tani moja ya dawa za binadamu na mifugo zenye thamani ya shilingi milioni 26.7 na tani 12 za vipodozi ambavyo thamani yake ni shilingi milioni 138.6.

Mwakilishi wa Afisa afya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Audax shilinde,anasema bidhaa hizo zimeharibiwa kutokana na uwezekano wa kuisababishia jamii madhara kwani viwango vya ubora wa bidhaa hizo pamoja na usalama wake kwa watumiaji unakinzana na matakwa ya sheria namba 1 ya chakula,dawa na vipodozi ya mwaka 2003 na sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009.

Bidhaa hizo zimeteketezwa katika dampo la jiji la Mwanza lililopo Buhongwa ikiwa ni utekelezaji wa sheria namba 1 ya mwaka 2003 ya chakula,dawa na vipodozi ambayo inalenga kudhibiti ubora,usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa,vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.
 
Back
Top Bottom