Mwanza: Polisi Wameua majambazi sita

Mwanza: Polisi Wameua majambazi sita

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,421
Reaction score
31,922
Polisi yaua majambazi 6 huko fomagila Mwanza. Kamanda Msangi amethibitisha.

Taarifa kamili hazijatolewa kuhusiana na sakata hilo.kwa mlioko jijini Mza mnaweza kutujuza zaidi.

Inasemekana ni tukio la kwanza kwa majambazi wengi kuuawa kwa mkupuo jijini Mwanza.

Chanzo: ITV

--
Watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi katika mtaa wa Fumagila Mashariki Kata ya Igoma jijini Mwanza.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo baada ya watu hao kuzingirwa katikati ya majengo mtaani hapo na kufanya mashambulizi ya kujibizana risasi kwa muda mrefu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akaomba alitolee ufafanuzi baadaye kwa kuwa hivi sasa bado anaendelea kukusanya taarifa zaidi.

“Ni kweli hilo tukio hilo lipo, ila bado tunashughulikia naomba munipe muda nitataoa ufafanuzi baadaye,” alisema kwa ufupi Kamanda Msangi.

Shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni diwani wa Kata ya Kishili iliyo jirani na kata hiyo, Sospeter Ndumi amesema kurushiana risasi baina ya watu hao na polisi kulianza usiku wa manane hadi majira ya asubuhi.

Amesema katika majibizano hayo polisi walifanikiwa kuwaua watu hao na kukamata silaha mbalimbali za kivita walizokuwa wanazitumia.

Katika mtaa huo huo ndipo lilipotokea tukio la Desemba 3 mwaka jana ambapo polisi waliwakamata watoto 11 wenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka sita hadi 14 baada ya kuizingira nyumba moja kwa lengo la kuwakamata watu waliowahisi kuwa majambazi.

Mmoja kati ya watu watatu waliokutwa kwenye nyumba hiyo alikimbia baada ya kuwarushia polisi bumu la mkono, kabla ya polisi kuwadhibiti waliosalia kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa huo.

Kadhalika katika tukio hilo, watu watatu waliosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa na bunduki mbili aina ya SMG na AK47, magazine saba, bastola moja na risasi 183 vilikamatwa na polisi.

Baada ya polisi kuondoka katika eneo hilo, wananchi waliiteketeza nyumba hiyo kwa moto.
 
Hivi ni lazima kuwaua tu hakuna namna ya kuwafikisha mbele ya sharia ?! Tutafute namna yakuwafikisha mbele za sheria ili wawajibishwe

Cairo's
 
Hivi ni lazima kuwaua tu hakuna namna ya kuwafikisha mbele ya sharia ?! Tutafute namna yakuwafikisha mbele za sheria ili wawajibishwe

Cairo's

Kwa kuwa hujakutana na mkono wa jambazi mwenye silaha endelea kuhoji, omba Mungu yasikukute hutaamini macho yako. Ukipona utaelewa kinachoendelea ila ikitokea jambazi kafanya yake jua umeacha balaa kwa familia.
 
K



Kwa kuwa hujakutana na mkono wa jambazi mwenye silaha endelea kuhoji, omba Mungu yasikukute hutaamini macho yako. Ukipona utaelewa kinachoendelea ila ikitokea jambazi kafanya yake jua umeacha balaa kwa familia.
Najua machungu hayo yanayotukuta lakini pia tusiwe taifa la kuua tu.

Cairo's
 
Kuna vitu havijakaa sawa, hivi si ni Mahakama pekee ndio yenye kutupatia majibu Kama MTUHUMIWA ana hatia au la[emoji780]Lkn now days ni kawaida JESHI la POLISI kutupatia Taarifa KUWA waliowaua ni MAJAMBAZI, kazi ya ku-arrest inafanywa na nani NA kufasiri sheria inafanywa nani? Kama. WEWE KE Fanya shughuli zako za ME hazkuhusu, AMA nimekosea[emoji780]
 
Haijaa vizuri kamwe,yale mafunzo ya ukamataji yamewekwa kando.
 
Safi Wauliwe tu maana hawa jamaa wanauwa ndugu zetu kibiti bila hatia, Jambazi unaua M/kiti wa kijiji amekusea nini???
 
Yawezekana maana jana mida Fulani hivi mishale kama 10-11:30 niliona gari za polisi kama 3 zikiwa zimebeba askali zinapita hii barabara ya kuelekea Airport ila sikufatilia kilichojili huko.
 
Back
Top Bottom