Mwanza na janga la maji

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,256
Reaction score
1,746
Nianze na nukuu kutoka Kwa gwiji wa muziki wa reggae, hayati Robert Marley aliposema" katikati ya maji, maji mpumbavu ana kiu"

Kwa muda wa wiki mbili Sasa maeneo mengi ya jiji la mwanza hakuna huduma ya maji na mamlaka husika hazichukui hatua zinazostahili.

Mamlaka hizi, mwauwasa na Ewura hawaoni taabu inayowakabili wakazi wa jiji hili lililoko kandokando ya ziwa Victoria!
Kwamba, tumezungukwa na maji lakini hatuna maji ni jambo lisiloingia akilini!
Mwauwasa wametumia mamilioni kujenga jengo jipya la ofisi zao wanaloita maji house huku wateja wake hawana maji!
Kwao ni Bora jengo jipya la ofisi lakini sio kuanzia kituo kingine cha kuchukua maji zaidi kilichopo Capri point, kilichoachwa na mkoloni wakazi mwanza ukiwa na idadi ndogo ya watu.
Leo hata ule utaratibu wa kutuma SMS Kwa wateja kuwaeleza juu ya tatizo lililoko, mmesitisha.
Ewura ninyi mnachojua ni kukusanya fedha zetu kupitia Ankara za maji lakini hakuna mnachofanya tukaona umuhimu wenu.

Ama Kwa hakika kama sio mvua hizi tungewashuhudia wanawake na watoto wakikata mitaa kuelekea ziwani kutafuta maji

In abundance of water the fool is thirsty
 
Nenda kachote ziwani au kinga maji ya mvua acha kulialia kama mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…