Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa usambazaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa
"Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kuwa kuna watu wawili wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani", alisema Sianga
Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano kila siku na kwamba hata leo, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa
"Leo asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa za kulevya, tupo naye tunaendelea kumhoji, mengi yataibuka "amesema Kamishna Sianga
Chanzo: Dar24