MWANZA: Majambazi yapora mamilioni kiwandani, Watatu wakamatwa

Mpaka nafika mwisho sijaona TRA wakitajwa kufika hapo kiwandani kufatilia kodi yao. Kama kina uwezo wa kukusanya fedha hizo kwa siku, kimelipa kodi stahiki? Au ni wahujumu uchumi kwa kutunza fedha haramu?
 
Kamanda Msangi amesema watu hao walikamatwa na fedha halali za Kitanzania Sh40 milioni na Dola za Marekani 190,000 na silaha aina ya Short gun vilivyoibiwa katika kiwanda kinachojihusisha na biashara ya mabondo ya samaki cha Weish AST Ltd jijini hapa.

Amewataja watu hao kuwa ni Seif Waziri (37), Daud Mwakalinga (35) wote wakazi wa Dodoma waliokamatwa wakiwa mkoani Singida wakiwa wamebaki na Sh2 milioni na Dola za Marekani 20,000.

Aliyeelewa kuhusu hizo pesa ilivyoandikwa naomba anielewesha.

Hapa kazi tu, hongera kwa mapolisi. Lazima kuna mtu wa kiwandani aliyewapa dilu hilo.
 
Wizi ni kazi ya laana. Pesa zote hizo na hawajafanya jambo la maana. Ukiangalia tangu waanze ujambazi hawana hata nyumba.
Pesa ambazo huzitafuti kwa jasho huisha km pande la barafu kwenye jua
 

Mwanza.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora Sh464 milioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana Alhamisi, Agosti 3 kuwa watu hao walikamatwa Julai 19 mwaka huu mkoani Singida walipokimbilia baada ya kufanya uhalifu.

Kamanda Msangi amesema watu hao walikamatwa na fedha halali za Kitanzania Sh40 milioni na Dola za Marekani 190,000 na silaha aina ya Short gun vilivyoibiwa katika kiwanda kinachojihusisha na biashara ya mabondo ya samaki cha Weish AST Ltd jijini hapa.

Amewataja watu hao kuwa ni Seif Waziri (37), Daud Mwakalinga (35) wote wakazi wa Dodoma waliokamatwa wakiwa mkoani Singida wakiwa wamebaki na Sh2 milioni na Dola za Marekani 20,000.

Pia amesema watu hao walikutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 011765714 na car namba 00107210 vitu vilivyoporwa jijini Mwanza. Mwingine ni Emmanuel Mwakilili aliyekamatwa jijini Mwanza baada ya kutajwa na wenzake.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi tukio hilo la uporaji lilitokea jijini Mwanza Julai 14, mwaka huu ambapo majambazi watano walivamia kiwanda hicho wakiwa na silaha za jadi na kumpiga mlinzi na kitu kizito kichwani na kumpora silaha kisha kuingia ndani na kupora kiasi hicho cha fedha na kutokomea kusikojulikana.

Amesema polisi walipokea taarifa za kiintelijensia kuwa majambazi hao wamekimbilia mkoani Singida ndipo askari walikwenda wakishirikiana na wamkoa wa Singida na kufanikiwa kuwatia mbaroni wawili.

“Baada ya mahojiano ya awali walipoletwa Mwanza, majambazi hao walikiri kuhusika na tukio hilo kisha walionyesha walipokuwa wameficha silaha na kumtaja mwezao amabaye naye alikamatwa,” amesema Kamanda Msangi.

Chanzo:
Mwananchi
safi sana,ukimkamata utajua na washirika wake,ukumua hutajua washirika wake.
 
Hao askari wakipelekwa kibiti watasaidia kuwapata watuhumiwa wa kibiti wakiwa hai maana hawa wa kibiti kazi yao ni kuua tu
Kwasababu hao wahalifu wa kibiti na wao kazi yao kuuwa tu askari na raia.
Si unajua hii kitu -> "Only one eye for one eye", also known as "An eye for an eye", or the law of retaliation, is the principle that a person who has injured another person is to be penalized to a similar degree.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom