MWANZA: Majambazi yapora mamilioni kiwandani, Watatu wakamatwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,511
MAJAMBAZI+PICHA.jpg

Mwanza.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora Sh464 milioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana Alhamisi, Agosti 3 kuwa watu hao walikamatwa Julai 19 mwaka huu mkoani Singida walipokimbilia baada ya kufanya uhalifu.

Kamanda Msangi amesema watu hao walikamatwa na fedha halali za Kitanzania Sh40 milioni na Dola za Marekani 190,000 na silaha aina ya Short gun vilivyoibiwa katika kiwanda kinachojihusisha na biashara ya mabondo ya samaki cha Weish AST Ltd jijini hapa.

Amewataja watu hao kuwa ni Seif Waziri (37), Daud Mwakalinga (35) wote wakazi wa Dodoma waliokamatwa wakiwa mkoani Singida wakiwa wamebaki na Sh2 milioni na Dola za Marekani 20,000.

Pia amesema watu hao walikutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 011765714 na car namba 00107210 vitu vilivyoporwa jijini Mwanza. Mwingine ni Emmanuel Mwakilili aliyekamatwa jijini Mwanza baada ya kutajwa na wenzake.

Kwa mujibu wa Kamanda Msangi tukio hilo la uporaji lilitokea jijini Mwanza Julai 14, mwaka huu ambapo majambazi watano walivamia kiwanda hicho wakiwa na silaha za jadi na kumpiga mlinzi na kitu kizito kichwani na kumpora silaha kisha kuingia ndani na kupora kiasi hicho cha fedha na kutokomea kusikojulikana.

Amesema polisi walipokea taarifa za kiintelijensia kuwa majambazi hao wamekimbilia mkoani Singida ndipo askari walikwenda wakishirikiana na wamkoa wa Singida na kufanikiwa kuwatia mbaroni wawili.

“Baada ya mahojiano ya awali walipoletwa Mwanza, majambazi hao walikiri kuhusika na tukio hilo kisha walionyesha walipokuwa wameficha silaha na kumtaja mwezao amabaye naye alikamatwa,” amesema Kamanda Msangi.

Chanzo:
Mwananchi
 
MAtatu, hapo kwenye "ma" kuna tatizo. Ukisema watatu stori hainogi????
 
Hao askari wakipelekwa kibiti watasaidia kuwapata watuhumiwa wa kibiti wakiwa hai maana hawa wa kibiti kazi yao ni kuua tu
 
Nalipongeza geshi.. Kazi njema sana hii.. Natamani majambazi yangerusha risasi ili polisi wapate sababu ya kuyamaliza kabisa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom