MWANZA: Jambazi auawa katika majibizano ya risasi na polisi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari Polisi waliokuwa doria katika mtaa wa Ilemela jijini Mwanza jirani na kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Mwanza Fishing LTD kufuatia majibizano ya risasi,huku majambazi wengine wawili wakifanikiwa kutoroka baada ya kuzidiwa nguvu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi,amesema tukio hilo limetokea Mei 31 majira ya saa 4.10 usiku,baada ya askari polisi waliokuwa doria katika maeneo hayo kuwatilia shaka watu watatu waliokuwa wakipita katika barabara iliyopo kati ya kituo cha Radio Free Afrika na kiwanda cha Mwanza Fishing ambao walikuwa wamebeba begi na askari walipowapa amri ya kusimama ili waweze kuhojiwa pamoja na kupekuliwa hawakutii amri hiyo.

Hata hivyo baada ya jambazi huyo kuuawa,askari walikagua bunduki na kubaini kuwa namba za bunduki hiyo aina ya Short machine gun,( SMG ) zilikuwa zimefutika na risasi 16 zilikutwa ndani ya magazini,huku begi likiwa na jaketi kubwa hali iliyoashiria kwamba watu hao walikuwa wamejipanga kwenda kufanya uhalifu mahali kwingine,mwili wa marehemu upo katika hospitali ya rufaa Bugando kwa utambuzi ambapo upelelezi na msako wa kuwakamata waliokimbia bado unaendelea.

Katika tukio jingine,mwanafunzi wa Chuo cha mipango ya maendeleo vijijini Kanda ya Ziwa kituo cha Mwanza Frank Chambi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mkazi wa Bwiru Dotto Japhet aliyeuawa kwa kupigwa na jiwe kichwani.

Chanzo: ITV
 
Mkuu, smg sio short machine gun ni submachine gun. Naijua kama sijui nini, nimelindia jakata, nimecheza nayo RTS, nimejira nayo levo3, nimecheza nayo cadet.....
 
Mwanza kwa matukio naona safari hii wapo juu. Pongezi kwa askari japo kuua inatakiwa iwe option ya mwisho. . Tunapowaua mnaacha kupata mtandao mzima.
 
Mwanza sio salama kabisa miaka ya hv karibuni..!! Nadhani majambazi wengi wanatoka nchi za jirani, Burundi, Kongo na Rwanda.. pia silaha za kufanyia uhalifu zinatoka kwa wingi huko, dawa ni kudhibiti mipaka na wahamiaji haramu..!!
 
Yani sikuizi jamani mwanza kila siku majambaz mala wamekamatwa bugalika mala wamechinja watu msikitini mala Fulani kavamiwa na kubakwa sijuwi tutaishije sasa
 
Jana nilisikia hiyo milio ya risasi ilikuwa mapema mnoo. Hali ni mbaya sana hatulali kwa amani.
 
Back
Top Bottom