Yule anayelinganisha Mwanza na Arusha ni mwendawazimu. Mwanza usilinganishe na vitu vya ajabu. Mimi Arusha na Mwanza kote nimefika tena sio kusalimu ndugu hapana ni kutalii kwamaana kwamba haya majiji yote nimezunguka vya kutosha. Kwakweli Mwanza ni level zingine aisee. kuna sehemu nyingi zinazopendeza. Nilifurahi sana nilipotembelea Saanane Island National Park kuliko mbuga ingine yoyote kati ya nilizotembelea, nilienjoy sana nilivyoenda Jembe ni Jembe Beach Resort....nilienda pia Tunza Beach Resort nilifurahi mnooo. Nikaingia Rock City Mall kutizama cinema...waachaa.
Majengo ya ajabu yapo Mwanza aisee kama lile jengo ukiwa unaelekea Saanane National Park (limejipindapinda hiviii).
Lakini kuna vitu pia viliniboa vinafaa virekebishwe kama aina ya usafiri wa vipanya, pia jiji linapoa mapeema mno...saa tano usiku kimyaa.
Sent using
Jamii Forums mobile app