Asante mkuu kwa kunikumbusha, niliwahi fikiria hilio. Tatizo ni viongozi wetu. Sababu za kukua kwa kasi mji wa DSM, ni kushindwa kuweka magawanyo sawa wa huduma za jamii. Angalia, kanda ya ziwa hakuna hata university yoyote ya serikali, ukiachilia SAUT na Tumain branch Bukoba. Ili upate elimu ya versity unalazimika uteseke kuja Dar, ukimaliza shule mawazo yako yote yanajua Dar ndo maisha. Binafsi, sipendi, sitamani kuishi dar. Nikija huwa nakaa siku mbili tu na kurudi peponi Mwanza. mwanza ni pazuri, rafiki zangu wakija huwa wanashangaa sana uzuri wa mwanza. kwa wajasiriamali ni jiji zuri sana, you can become rich within a very short time.
Ushauri: serikali ifungue vyuo kama dodoma kilia mkoa wa kanda ya ziwa, ueone kama watu watarundikana dar. I Love Mwanza.