Mwanza: Amuua mke wake kwa kumpiga risasi, naye ajiua

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.

Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .

Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
 
Fundisho:
Mkishaoana muache mambo mengine ya ajabu ajabu ambayo huleta uadui. Maana unapokwenda kinyume na mwenzako huwezijua moyoni mwake na akili yake inakuwaziaje!!!!
Hii ndiyo hatma ya kutoelewana katika maisha ya wanandoa.
 
Daah pole kwa wafiwa, Morogoro nako pia mume kamuua mkewe na kutumbukiza mwili mtoni, kisa ameombwa pesa ya matibabu ya mtoto.
 
Kujitoa uhai na kutoa wa mwingine pia ni kosa la jinai na analakujibu mbele za Mungu, wakati mwingine ni vyema umilikishwaji wa silaha upewe vigezo zaidi kwa majaribio ya mara kwa mara kabla ya kukubaliwa umiliki
 
mwananchi.PNG


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom