Mwangunga aanza kampeni kuwania Jimbo la Ubungo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Na Salim Said

KAMPENI za kuwania Ubunge Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam zimeanza kwa kasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga kumwaga fulana na vitambaa vyenye picha yake kwa wanachama wa chama hicho wakati akisimikwa kuwa Kamada wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata.

Mwangunga ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na mbunge wa kuteuliwa, ni mmoja kati ya vigogo wa CCM wanaotarajia kugombea Jimbo hilo la Ubungo lenye upinzani mkali ndani na nje ya chama chake.

Hali hiyo inatokea wakati CCM wala Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), hazijatangaza kuanza kwa kampeni za uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.

Diwani huyo wa Ubungo, William Masanja aliitisha mkutano huo juzi, kwa ajili ya kumsimika Mwangunga kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM kata hiyo, huku akiutelekeza uongozi wa chama na wa vijana katika kata ambao ndio walengwa.

Shamra shamra za hafla hiyo zilipambwa na maandamano ya vijana waliovaa fulana na vitambaa vyenye picha ya Mwanguna na kusindikizwa na kikundi cha matarumbeta kutoka Tabata, yaliyoanza katika kituo cha Daladala cha Rombo hadi katika uwanja wa mpira wa Kibo Ubungo.
 
Mwanyika yule aliekuwa Mwanasheria mkuu?
I bet mkuu alilenga kusema "Mnyika" akachanganya madawa. Tatizo la maandishi ukikosea herufi moja tu unamaanisha kitu kingine kabisa.

So far, najaribu kufikiria wabunge wa kuteuliwa katika vyama vyote kama wataweza kuambulia kitu katika "Season Finale" (2010 - 2015) ya JK, kazi ipo!
 
Mnyika is right person for Ubungo na pia itakuwa ni vyema kama wana unbungo watafanya hivyo
 
HAINA NENO DAR HAINA MWENYEWE TOFAUTI NA KULE KWETU AMBAKO UKITAKA UBUNGE ITAKUBIDI MPAKA UONYESHE ALIPOZIKWA BIBI YAKO, BABU YAKO KAMA HAITOSHI MKE /MUME WAKO NI RAIA WA NCHI GANI.....NA WAZAZI WAWE NA KUMBUKUMBU NA WAONYESHE KITOVU CHAKO KILIzZIKWA MAENEO GANI PALE SHAMBANI

Ni kweli keenja amepwaya pale stendi ya mkoa! Mnyika nikikuangalia usoni kama unanipa matumaini maana Nyerere alisema hatuna budi kumwangalia mtu anaetaka kuwa kiongozi wetu usoni na kuona kama MANENO YAKE na matendo vinakwenda pamoja. Ila sasa mdogo wangu endeleza utii hapo CHADEMA maana naona kama upepo kwa vijana hauko shwari wasije wakakuzalishia majungu watu wasioipenda nchi yetu na wakubwa bila kujali wakaku KABA usigombee! sawa! eeeh ishi kwa ujanja kidogo muda uliobaki si mrefu. Ni ushauri tu unaweza kutoufuata kama hauna tija sawa JM
 
Huko Ubungo kazi ipo!

Mdogo wa Waziri Nchimbi ajitosa Ubungo


na Andrew Chale


MDOGO wa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi, aitwaye Alfred John Nchimbi (39), jana ameongeza idadi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wenye nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Ubungo mwakani.

Alfred Nchimbi, ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Muhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma (Magogoni), alitangaza azima yake ya kugombea ubunge katika jimbo hilo, alipozungumza na waandishi wa habari jana, muda mfupi baada ya kufungua semina ya mafunzo ya siku moja ya anwai za jamii.
Kada huyo alisema kuwa, ameamua kujitokeza kuitaka nafasi hiyo ili kupata fursa ya kuwaongoza wananchi waliokosa fursa ya kufanya maamuzi sahihi, huku wengi wao wakipitia kwenye maisha magumu na ya mateso.

"Wakati ukifika nitagombea. Naomba ridhaa ya chama changu ambao ndio walio na maamuzi ya mwisho na wakinikubali nitagombea," alisema Nchimbi.

Alibainisha kuwa ana uhakika wa kupata nafasi hiyo adhimu ambapo ataitumia kwa kupeleka maendeleo katika jimbo hilo pamoja na kuwakomboa wananchi ambao kwa miaka mingi hawajapata maendeleo yanayotakiwa.

Aliongeza kuwa, ametumikia chama kwa muda mrefu na kuiva katika siasa jambo ambalo anaamini litamsaidia kufanikisha maendeleo ya huduma muhimu zikiwemo za miundombinu, afya na ulinzi.

Nia hiyo ya Nchimbi, inakifanya kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo kuwa kigumu baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga kutangaza mapema kuwania kiti hicho. Mbali na Mwangunga, kuna taarifa za kuaminika kuwa kada kijana wa chama hicho, Nape Nnauye, naye ni miongoni wa watakaowania kiti hicho kinachoshikiliwa na mbunge wa sasa, Charles Keenja, ambaye naye huenda akakitetea tena kiti hicho. Katika uchaguzi mkuu uliopita, Keenja alichuana vikali na kada machachari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, na kupata ushindi uliogubikwa na mizengwe mingi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom