Mwanga: Basi la Kampuni ya Dar Express lagongana na Basi la Kampuni ya Esther Luxury Coach

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Watu kadhaa wamenusurika vifo kufuatia ajali iliyotokea maeneo ya Mwanga kwa kuyahusisha mabasi mawili ya kampuni ya Dar Express na Esther Luxury Coach kugongana.

Ajali hii namna ilivyotokea ni kwamba Esther Luxury na Dar Express walikuwa wamefuatana kwa karibu na walipofika eneo la daraja la kupita gari moja kulikuwa na gari tayari limeanza kuingia, dereva wa Esther Luxury Coach akasimama ndipo Dar Express ikaja kumvaa kwa nyuma.

Taarifa za awali kutoka eneo la ajali, hakuna vifo isipokuwa majeruhi tu.
IMG_20180923_154411_687.jpg
IMG_20180923_154428_828.jpg
 
muda huu ni muda ambao mabasi mengi huwa yanawahi ili yawahi kufika sasa kufuatana kwa karibu bila ya kujali meter za umbali kati ya basi na basi huwa unatokea sana maana ni uzembe wa madereva wengi wakiaminiana kuwa hawezi kusimama ghafla, sasa hapo ndio hivyo tena hamna jinsi ni hasara tu
 
Ajali imetokea maeneo ya Mwanga ikihusisha basi la kampuni ya Dar Express na Esther Luxury Coach kugongana.

Chanzo cha ajali hii bado hakijafahamika ila tutakujuza zaidi kadri inavyowezekana, taarifa za awali hakuna vifo isipokuwa majeruhi tu.View attachment 875456View attachment 875457


Ajali imetokea saa ngapi?
Ungeweka picha ya mwonekano wa mabasi husika yote kwa pamoja kutupatia ssura kamilinya tukio
 
Huyu dereva wa dar express ndo
Mwehu kabsa Sasa anamfuata mwenzake kwa ukarbu hvo
Kama co Bangi bhas n ulev wa konyag
 
Ajali imetokea saa ngapi?
Ungeweka picha ya mwonekano wa mabasi husika yote kwa pamoja kutupatia ssura kamilinya tukio
Imetokea mchana mkuu...Na picha mbona ziko sawa kama hiyo Dar Express inaonekana eneo lote la mbele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom