Mwandosya na Lipumba wafanyiwa upasuaji India

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Wamefanyiwa upasuaji(operation) katika hospitali moja nchini India ijulikanayo kama Apollo iliyopo mjini Hyderabad.
Prof Lipumba ana tatizo la figo na keshafanya upasuaji na alishindwa KUELEZEA hali yake kwakuwa dawa za usingizi
zilikuwa bado hazijaisha, akashindwa kuongea.
prof Mark Mwandosya anaumwa uti wa mgongo na kuna pingili moja ya mgongo imeoza, keshafanyiwa upasuaji na
yupo huko wiki ya pili sasa. Tatizo lilianza wakati yupo kwenye kikao cha bunge. Kapelekwa muhimbili lakini wapi.

Mungu awape baraka zake mpone haraka mje kutumikia taifa.

sosi: Gazeti(Mtanzania kama sio Tanzania Daima)
 
Mungu awasaidie wapone haraka wakapumzike Marekani baadaye waje tusaidie kuboresha mazingira ya madaktari wetu wa Muhimbili.
 
nashindwa kusema pole kwa mwandosya
maana yeye ni mmoja wa watanzania walioifikisha hapo
sector ya afya na huduma zake

masikini wengi wamekufa na magonjwa madogo madogo hali wao
wakilipwa maposho makubwa kama waziri kila nakokwenda analipwa milioni 1.2
kama posho, hata kama amekwenda kwenye semina ya wizara yake lazima walipwe

sasa hiyo pesa wanayokwapu tungeweza kuwa na hospitali za maana kwa ajili ya watanzania
wote, yeye sasa yuko india hapa nyumbani watu wanaendelea kufa hali wao ndio sababisho.

augue kwa kadri mungu apendavyo
 
Mwandosya kashapigwa jugna juhi!! Siasa bana!

wanajifanya wana tamaa ya uongozi lakini hawana personal security
wanadhani hii system ya usalama wa taifa inayomaliza watanzania wao haitowagusa
ngoja wamalizwe wakishituka wanapigana kurekepisha mfumo ili husinunulike au kumfanyia mtu dirty work
 
mwandosya anapenda kazi zionekane,pole mzee wa tukuyu
 
Na hao ni Class A citzen
Sasa sijui sisi class C na wale wengine Class D citzen wakipata matatio kama hayo ndo vipi. Unapewa panadol?
 
Na hao ni Class A citzen
Sasa sijui sisi class C na wale wengine Class D citzen wakipata matatio kama hayo ndo vipi. Unapewa panadol?

Class A flight, Class A vehicles(VX-V8)!! Class A bungeni!! Class A hospital...list ni ndefu sana! Ndio maana Mbowe kawachana bungeni live!! Wakistaafu hawa hata ndege hawapandi!! Bongo bana
 
Aaaa,wataalam wa muhimbili,bugando na kwingnwko wa nini?????ndio maana watumishi wa afya,walimu na wataalam wengine hawalipwi ipasavyooooo......mzee malecela alienda UK now amepumzka USA,nyerere alienda UK,
 
Hapa ndipo utaona kweli hospitali zetu magumashi roho mkononi!!

Tatizo kila kitu kimekuwa siasa, ulimwengu wote hauwezi kuwa sawa ndg. Kuna specialisation of labour.
Mfalme wa Saudi Arabia juzi alikuwa matibabu New York, rais wa Venezuella kwa sasa yuko Cuba kwa matibabu.
Sasa unashangaa nini wao kwenda India?
Mungu atawaponya.
Poleni sana
 
Back
Top Bottom