Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,752
MWANDOSYA, MGEJA WAMPIGA
KOMBORA SITTA
na Waandishi wetu
SIKU chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk.
John Magufuli, kumruka Waziri wa Ushirikiano
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta,
akisema hahusiki na kundi lolote la mbio za
urais mwaka 2013, Waziri Mark Mwandosya,
naye ameruka akisema Ikulu bado ina
mpangaji.
Wakati Profesa Mwandosya akimsuta Waziri
Sitta, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja,
amemshukia waziri huyo wa Afrika Mashariki
kuwa ni msaliti na anapaswa kufukuzwa kwenye
chama.
Viongozi hao waandamizi ndani ya CCM walitoa
kauli hiyo kwa wakati tofauti mjini Dodoma na
Mgeja akiitisha mkutano na wanahabari jijini
Dar es Salaam.
Kauli za viongozi hao zimekuja baada ya Waziri
Sitta hivi karibuni kuwataja mawaziri wenzake
watatu akidai kuwa ni marafiki zake, wasafi,
wasio walafi na wanaomuunga mkono katika
vita dhidi ya ufisadi.
Sitta ambaye anatajwa kuwa mmoja wa makada
wa CCM wanaotaka kuwania urais mwaka 2015,
aliwataja marafiki zake hao wiki iliyopita kuwa
ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Dk.
Magufuli na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe, kuwa wana mikono safi na si
kama wengine walafi na waongo
wanaowatumbukiza katika mikono ya Dowans
na Richmond ambao si waadilifu na wazalendo.
Licha ya kutomtaja mtu kwa jina lakini wadadisi
wa kisiasa wanasema kuwa alimlenga kada
mwenzake, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa huo mwaka
2008 kutokana na kashfa ya Kampuni tata ya
kufua umeme ya Richmond.
Lowassa ni miongozi mwa vigogo wa CCM
wanaopewa nafasi kubwa kuwania urais mwaka
2015 na kundi lake lenye nguvu linadaiwa
kuwapa kiwewe wapinzani wake ndani ya
chama.
Hata hivyo, siasa hizo za makundi na kuanza
kurukana kwa wajumbe tajwa huenda
zikamweka pabaya Sitta endapo atawania kiti
hicho.
CCM imekuwa ikiwaonya makada wake
wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali za
uongozi kutothubutu kufanya kampeni zozote
kwani muda bado na kwamba atakayekiuka
atakuwa amejiengua kwenye mchakato wakati
ukifika.
Jambo kubwa litakalomweka pabaya Sitta katika
siasa zake za kujiimarisha kuelekea mwaka
2015 ni kitendo cha marafiki aliowataja katika
harambee hiyo kuwa ni washirika wake
wanaomuunga mkono na kumchangia fedha
kuanza kumkana.
Sitta ambaye ametangaza kutogombea tena
ubunge, aliwasilisha zaidi ya sh milioni 25
ambazo alisema kati yake sh milioni tano
zilitoka kwa Membe, sh milioni tano nyingine
zilichangiwa na Dk. Mwakyembe na Dk.
Magufuli huku yeye (Sitta) akichangia sh milioni
tano.
Alitaja kuwa fedha zilizobaki ili kutimiza
mchango wake wa sh milioni 25 zilichangwa na
wabunge wanaowaunga mkono ambao ni Anne
Kilango, Mary Nagu, William Ngeleja, Aden
Rage na Catherine Majige.
Wengine ni James Lembeli, Mark Mwandosya
pamoja na Victor Mwambalaswa ambao wote
walimchangia sh 500,000 kila mmoja huku
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu akitoa sh milioni moja.
Hata hivyo, Magufuli amekuwa wa kwanza
kukanusha kauli ya Sitta akisema hakuwahi
kuchangia hata senti moja katika fedha
zilizotajwa.
Katika mlolongo huo, Tanzania Daima Jumapili
liliwasiliana na baadhi ya vigogo wa CCM
waliotajwa kumchangia Waziri Sitta, likitaka
kufahamu msimamo wao kama walifanya hivyo
kimkakati kuelekea urais mwaka 2015 au la.
Katika maelezo yake, Waziri Mwandosya
ambaye alichuana na Rais Jakaya Kikwete
mwaka 2005, alisema ana kundi moja liitwalo
CCM.
Niko nje ya nchi kwa hiyo sina taarifa ya hayo
unayoyasema kwamba yamesemwa. Hata hivyo
na kama ni kweli itanishangaza. Tuna kazi ya
kutekeleza ilani na ahadi zetu kwa wananchi wa
Tanzania. Magogoni (Ikulu) bado ina mpangaji.
Nilisema wakati ukifika Mwenyezi Mungu
akipenda, nitatoa uamuzi. Sihitaji msemaji wala
kusemewa. Mungu ibariki CCM, Mungu ibariki
Tanzania, alisema Profesa Mwandosya ambaye
ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (asiye na
Wizara Maalumu).
Naye Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa,
alijibu kwa kifupi kuwa: Mimi nilimchangia
laki tano kama rafiki. Mengine siyajui.
Mmoja wa mawaziri waliotajwa katika kundi
hilo, alipotafutwa aliomba apewe muda ili
aweze kutoa ufafanuzi baadaye.
Mwanzoni mwa wiki hii, Dk. Magufuli alikana
madai ya Sitta akisema kuwa hajawahi kuwa na
ushirikiano wa kumuunga mkono katika
masuala ya kisiasa wala hajawahi kumtuma
akaseme chochote.
Badala yake Magufuli alisema kuwa habari hizo
ameshangaa kuzisoma kwenye vyombo vya
habari wakati hajawahi kufanya makubaliano
yoyote na Sitta wala kuunda kundi la mbio za
urais mwaka 2015.
Naapa sijawahi kuzungumza wala kuhudhuria
mkutano wa kundi lolote la mgombea urais,
naomba Mungu aogopwe, watu wasiwasingizie
wengine. Mimi kundi langu ni CCM, alisema.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Magufuli alisema
kwa sasa Rais ni Jakaya Kikwete, hivyo ni
makosa kuanza kampeni za urais wakati muda
bado.
Mgeja naye amsuta Sitta
Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM wa
Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja,
amemshukia Waziri wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, kuwa ni msaliti na anatakiwa
afukuzwe kwenye chama.
Mgeja alisema Sitta amekuwa wakati wote
akiisaliti CCM kutokana na kauli zake zenye
utata na hata kudiriki kuanzisha chama ndani
ya CCM cha CCJ.
Mgeja, mmoja wa wenyeviti wenye ushawishi
CCM, alimshambulia Waziri Sitta kuwa
amekuwa akiunda makundi ndani ya CCM,
jambo ambalo alisema ni hatari sana.
Chama kilishakataza kujitangaza, yeye kwa nini
anapitapita makanisani na kujitangaza? Sasa
kuna haja ya kuongea na Waziri wa Mambo ya
Ndani ili apige marufuku viongozi wa siasa
kufanya mikutano ndani ya makanisa na
misikitini, alisema Mgeja.
Mgeja alisema anakusudia katika kikao kijacho
cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kumshitaki
Sitta ili ajadiliwe kama bado ana sifa ya kuwa
kada wa CCM.
Mgeja alimshangaa Sitta kuendelea kulalamika
kuenguliwa kwenye kuwania kiti cha spika,
huku akimhusisha Rais Jakaya Kikwete kwamba
alihusika katika mpango huo.
Sitta amekuwa akimtuhumu hata Rais Kikwete
kuhusika kumuengua kwenye uspika huku
akisahau kuwa hata yeye nafasi hiyo aliipata
kwa wao kumfanyia hila Pius Msekwa na
kumtaka marehemu Juma Akukweti kwa wakati
huo ajitoe katika kinyanganyiro hicho ili spika
awe Sitta.
Nasema hivi msimuone Sitta amekuwa mtu wa
kulalama, anakosa fadhila tu, sisi ndio
tuliomuweka pale kwenye uspika wakati ule,
maana hakuwa na ubavu wa kumuondoa Pius
Msekwa, lakini leo hii kasahau, hakutakiwa
kusahau, anatakiwa kuiga mfano wa Msekwa,
maana amekaa kimya, alisema Mgeja.