pambe samanini
JF-Expert Member
- Oct 27, 2015
- 368
- 169
Bahati mbaya sikusoma chekechea bali nilianza darasa la kwanza huku tukimba nyimbo za Kiswahili ambazo kwangu sikuweza kuimba kwa sauti badala yake nilikuwa nachezesha midomo ( lips) pamoja na kufungua kinywa changu kana kwamba natabasamu. Bahati mbaya mwalimu wangu hakujua kuwa sikusoma chekechea, baadaye tulianza kuimba a e i o u nazo zilinipa shida sana hasa mwalimu alipofafanua kuwa e ipo kama jicho, o kama yai, u kama kikombe ikanibidi kukariri, ajabu sana tulipoanza kuandika chini mwalimu alinipongeza nilivyo kuwa naunganisha herufi mithili ya mikorogo ya kinamama. Mwalimu hakujua shida yangu, mwalimu alituagiza daftari na penseli lakini mwalimu alinichagua kuja na kalamu ya wino, nilipofika nyumbani niliwaeleza baba na mama kuhusu maagizo ya mwalimu wazazi wangu walinipongeza kwa uwezo wangu mkubwa tofauti na wanafunzi wenzangu laiti wazazi na mwalimu wangelijua shida yangu wangenirudisha chekechea bahati mbaya wazazi wangu hawakwenda shule naye mwalimu alikuwa wa UPE hakujua ubaya wa MWANDIKO wangu kutokana na yeye hakujua kuandika vizuri hapo ndipo mwalimu aligeuka kuwa rafiki yangu, baadhi ya wanafunzi wenzangu walinichukia kwani walisema nimebebwa wala sina akili kuzidi wao nami niliwaambia wacha nibebwe pamoja na akili yangu ndogo; hadi sasa ni kiongozi Mkuu katika taifa langu huku mwalimu wangu ndiye tunayefanya naye kazi. Je MWANDIKO wangu una maana gani?