Mwanaume usithubutu kumpa mwanamke moyo wako wa thamani, mpe hela sio moyo.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Mauaji ya mapenzi yanazidi kushika kasi kila siku, mauaji ya mapenzi yamekuwepo miaka na miaka ila sababu ya teknolojia sasa yanaonekana ni jambo geni kwa sababu ya uharaka wa kusambaa taarifa.

Mauaji mengi wanawake wanaonekana ndio victim wakubwa, takwimu za kesi za mauaji toka jeshi la polisi linaonyesha mikoa ya kanda ya kati na kaskazini naongoza katika kesi zote za mauaji.

Msingi mkuu wa mauaji haya ni wivu wa mapenzi, mmoja kumlaumu mwenzake kumsaliti au kumuacha bila kutegemea.

Niwashauri wanaume wenzangu, ili usije kujikuta kwenye matatizo kama haya ya kujiua au kuua mtu sababu ya mapenzi. Mwakamke mpe hela kadri uwezavyo ila sio moyo. Usije kuthubutu kumpa mwanamke moyo wako.

Sisi wanaume kwenye mapenzi hua hatupendi pendi kama wanawake ambae anaweza kuachwa leo kesho akapenda bila shida, sisi tukipenda hua ni mars moja na kwa dhati, tukiumizwa inaweza kutuchukia miaka tena kupenda au tusipende tena hadi kifo. Upendo wetu ni wa thamani sana, pale tunapoamua kumpenda mtu hua tunajitoa sadaka kwa ajili yake, we dedicate amd sacrifice all for her. Sasa ikitokea tumesalitiwa baada ya kupenda hua tunavurugwa sana na wengine hufikia hatua ya kushindwa kuhimili maumivu ya usaliti hivyo kua na option 2, kujiua au kuua mhusika au kuua mhusika na kujiua kwa pamoja(hizi ndizo option za wanaume wengi walioshindwa kuhimili maumivu ya mapenzi).

Lazima pia tuelewe mwanamke ni mtu anaongozwa zaidi na hisia, anaweza kukupenda leo na kesho asikupende bila sababu tofauti na sisi tukipenda tumemaliza.

Sasa, ili kuepuka hayo, nawashauri wanaume wenzangu, usithubutu kumpa mwanamke moyo wako, mpe hela kadri uwezavyo ila sio moyo, moyo wako ndio maisha yako, mtu akivuruga moyo wako anavuruga maisha yako. Usiuchezee kamari moyo wako.

Huu ni ushauri wa bure tu natoa kwa wanaume wenzangu.
Ushauri wa bure kwa wanaume wenzangu, mwanamke mpe hela, usimpe moyo wako, utakuja kujuta. - JamiiForums
 
Umenena hawa viumbe ambao hadi vitabu vya Mungu vinasema tukae nao kwa machale ni hatari kwa maisha na afya zetu , natamani nojiunge na QT ya upadri niepuke kikombe hiki ( wanawake)
 
Kwakweli mtupe tu pesa

Moyo hata n'gombe anao

Obvious jamaa hajaweka vizuri hoja mtu akikupa pesa pia moyo wake upo kwako hapa nazungumzia pesa endelevu

Kwahiyo huwezi kutenganisha moyo wa mtu na pesa vinakwenda sambamba.

Nb. Hakuna raha hapa Duniani kama kutumia hela yako na mtu unayempenda
 
Obvious jamaa hajaweka vizuri hoja mtu akikupa pesa pia moyo wake upo kwako hapa nazungumzia pesa endelevu

Kwahiyo huwezi kutenganisha moyo wa mtu na pesa vinakwenda sambamba.

Nb. Hakuna raha hapa Duniani kama kutumia hela yako na mtu unayempenda
Ahaaaa kumbe iko hivi... Ngoja nitafute anipendae tutumie wote dollari
 
Obvious jamaa hajaweka vizuri hoja mtu akikupa pesa pia moyo wake upo kwako hapa nazungumzia pesa endelevu

Kwahiyo huwezi kutenganisha moyo wa mtu na pesa vinakwenda sambamba.

Nb. Hakuna raha hapa Duniani kama kutumia hela yako na mtu unayempenda
Kufa kwa asili sio kujinyonga au kuua.
 
Hao wanaume wanaoua wanapenda pesa sio wanawake
Wanaua si sababu ya upendo ila kile walichowekeza kwa mwanamke!(Pesa ndiyo iko mioyoni mwao)
Chunguza malalamiko ya hao wauaji kama kabahatika kuongea hasemi upendo atasema nimepoteza hela zangu nyingi na muda wangu mwingi.
 
Wazee wetu walifaidi Sana
Sisi wa kizazi cha technology shida tupu

Unampenda anakuona Zoba
Ukimfanyia vitibwi anakuona humdhamini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom