Mwanaume tambua dawa ya wanawake wanaokukataa kwa sababu huna pesa

nyaggad

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,160
693
Habari wandugu,

Natumaini mko poa,kuna tabia ambayo baadhi ya wanaume wamekuwa waki wa lalamikia wasichana kuwa hawana mapenzi ya Kweli wanapenda pesa tu,sasa minawapa dawa wanaume wenzangu ya kufanya wanapokataliwa na wanawake kwa sababu ya kipato chao kidogo,mwanamke akikuka taa kwa sababu huna pesa,usilalamike wala kusononeka,unachotakiwa kufanya tafuta pesa kwa nguvu zako zote"focus "kwenye malengo yako ya mafanikio mpaka ufanikiwe na wwe siku ukifanikiwa ukiwa tajiri,wanawake maskini wakikushobokea wakijifanya wanakupenda usiwakubalie na kamwe usikubali tena kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke maskini au mwanamke njaa wao si walikukataa ulipokuwa huna kitu,na ukioa oa mwanamke tajiri usioe mwanamke maskini wasije wakakurudisha nyuma kwa sababu wanawake wengi wanaopenda wanaume matajiri hawajui "struggling" wanapenda short cut na hawana vision zao binafsi za kufanikiwa zaidi ya kutegemea wanaume ndio wawatoe kimaisha.

Fanya kama alivyofanya Diamond platinum alipokuwa hana kitu wanawake wazuri walimkwepa kama ukoma alipozipatatu akawa gumzo kwa wasichana mjini,kila msichana anajifanya anampenda Diamond platinum, alipokuwa hana kitu mbona walimtenga,ila nimemsifu ameoa mwanamke tajiri tena kutoka nchi za nje,zari the boss lady,na wwe ukizipata oa hata mtoto wa Obama,kwanza ukifanikiwa ukawa tajiri usioe kabisa mwanamke maskini wanawake wengine wana mikosi utafilisika bure,na Rudi kwa wasichana wanaopenda wanaume matajiri na kuwapiga chini wanaume wenye kipato cha chini.

Kama wwe ni msichana unapenda wanaume matajiri na kushauri tu uache hizo tamaa zako kwa sababu kwanza unatakiwa ujue wanaume matajiri wapo wa chache kwa hiyo sio rahisi kuwapata wakakuoa ni bora ukomae tu na maskini wenzio ipo siku mnaweza mkatoka,pili asilimia kubwa ya wanaume waliofanikiwa walikuwa na wapenzi wao Tangu zamani, kuna usemi unasema "kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke shupavu" kwa hiyo wwe kama msichana sio rahisi kuwapata wanaume matajiri wakakuoa labda wakutumie tu kama chombo cha starehe,na choku washauri komaeni na maskini wenzenu mtatoka tu shida zina mwisho wake mkiji tuma.

Note: no short cut to process.
 
Mkifocus kutafuta hela ndo wanawake tunakua tumefanikiwa make lengo letu ni kuwafanya mzitafute....
 
Kweli kuna wanawake wana destiny ya umasikini

sio kama atakufilisi ila mtafilisika wote
 
Biblia inasema usimpe moyo wako mwamke alalaye kifuani pako!
Yaani usimfungukie mambo yako yote muhimu kwani utapotea.(Naturally weak!)
 
Ulianza kutoa ushauri vizuri but ukaanza kuharibu kwamba tusioe masikini.

Kwa hapo nakupa 20/100 kwa ushauri wako...
 
Usiwe kama hayawani unazungumzia umaskini?au uzuri?mtu huna kitu utapataje dem mkali babu?? Nenda kwenye size yako.Au tongoza maskini wenzio.Mkono mtupu haulambwi babu.
 
Back
Top Bottom