Mwanaume mwenzangu usioe mwanamke aliyekuzidi uchumi/Hela utanyanyasika na kufa mapema

Mmhh maswala ya wanaume kula kwa jasho la wake zao ndo hamjui makubaliano yao ila maswala ya wanaume kusaidia wake zao kazi za ndani ndo roho huwa zinawauma
Najibu kadiri unavyoniuliza,I'm not responsible for what other members said or think.
 
Kwani sisi wanawake kuna sehemu kwenye maandiko tumeagizwa kula kwa jasho letu au kuhudumia familia?
Haijaandikwa, ila pia ni exclusive kwa walioolewa tu. Kama huna mume huwezi kukwepa kula kwa jasho lako
 
Mwanamke anakunyanganya simu, wewe utakuwa mwanaume wa Dar . Mwanamke akikupa hela mwanaume kuna mawili either anapewa na mwanaume mwingine ( WENGI WAPO KUNDI HILI) au ni hela za familia. Kama ni kundi la kwanza tegemea dharau, kejeli, fedheha mda wowote kwani stress za mahusiano yake mengine yote atamalizia kwako kwani baada ya muda yatamchosha lakin hatakuwa na namna ya kuyaacha( WEWE HUNA UWEZO WA KUMFANYA AISHI VIZURI).

All in all mahusiano kati ya mwanamke mwenye kipato kikubwa zidi ya mwanaume mwenye kipato cha chini yanaweza dumu tu pale ambapo chanzo cha mapato cha mwanamke ni biashara binafsi/familia na sio kutoka kwa mwanaume mwengine bila kusahau mwanamke awe anampenda huyo mwanaume kweli (UNCONDITIONAL LOVE).
Eti unconditional love?nyoooo
Hakuna mwanamke anafurahia hela yake kutumiwa na mwanaume,tena especially niwe nimeitafuta mwenyewe kwa jasho,patachimbika
Baadhi ya mijanaune ya sikuhizi yanapenda mteremko
Binafsi mwanaume akila hela yangu na heshima inashuka,hata Kama tunadate tu,na nitajiondoa kwenye hayo mahusiano haraka sana
Mwanamke hajaumbwa kulea dume lenye kengele zake bana,jiongezeni
 
Mfano wako ni mzuri sana ndiyo siwezi kumjibu shit kwa sababu yeye ndo boss na yeye ndo ananipa mshahara siyo mimi ninayempa mshahara sasa vipi kwa kwa wale wanaume (maboss) ambao hawahudumii wake zao (hawawalipi mshahara wafanyakazi wao)?
Hapo ndipo dhana ya kiburi ilipojificha, kuna nyakati ambazo hata mshahara pia hucheleweshwa japo mmefanya kazi yenu tayari. Mbona hamuachi kazi kwa kiburi kwamba hamjalipwa?

Translation: Mume wako unahisi unammudu sana ndio maana unataka umuendeshe unavyotaka, ndoa sio kitu cha maana kwako.

Mume kukuhudumia ni swala mtambuka, lazma afanye hivyo ilihali ana uwezo sana. Ikiwa hana uwezo basi walau afanye yale yalio ndani ya uwezo wake na ukiona mumeo hakuhudumii kuna mambo mawili aidha hakupendi, au hana uwezo.
 
Inasikitisha sana
I feel so sorry for those women
Ndoa hazina raha hizo.,zingekuwepo wasingekua wanahangaika nje
Zinayo sana,si ndo wanawake wenye elimu ndogo na wasiochangia lolote kwenye uchumi wa familia ambao wanaume ndo wanawataka
Lengo hasa ni kuwanyanyasa na kuwafuja,mtu hata hela ya kujinunulia lotion hana ataacha kupauka hahahah
 
Ili kuepuka kulishwa ndiyo maana
1. Huwa hatuoi mwanamke aliyetuzidi kipato au elimu.
2. Kama ukinizidi kipato kwenye familia halafu huniheshimu huwa tunavunja ndoa tunaoa mke mwingine ambaye ninamzidi kipato sababu atanieshimu. Si nina pesa, utanisumbua nini
3. Kama mambo yakienda kombo halafu sina kitu huwa tunakimbia familia ili kuepuka uliyosema. Badala umshauri mumeo unamcheka.
N.B
Kwa mwanamke kama wewe, unayemcheka mumeo ambaye ameanguka kiuchumi wakati alipokuwa na mali ulizitumia. Badala umfariji na umshauri nini afanye unaanza kumcheka. Unategemea utamheshimu ukizimdi kipato? Ndiyo maana huwa hatuoi aliyetuzidi kipato bora unizidi elimu na siyo kipato sababu za dharau kama zako. Tunawajua wanawake vizuri na huwezi kukuta mwanaume rijali anaoa mwanamke anayemzidi kipato.
Wanaume nguvu zetu zipo kwenye elimu na pesa ndiyo maana huwa hatutaki kuwa wanawake kama The iron batterfly na ikitokea, basi tukiishiwa huwa tunakimbia familia sababu tunaamini "mwanamke hana cha kukupa zaidi ya uke wake tu"
Ndo anachosema mleta mada,oeni wanawake size zenu msiparamie wanawake wenye elimu na wanaojiweza kiuchumi mtegemee kutunza
Mtapewa dharau Kama zoteeee
Mie siwezi kuwa na mwanaume nayejua namzid elimu ama visenti,kwa roho niliyonayo ya kujitoa na kuhudumia family na kuona Mambo yanaenda najua ataona kapata mtelezo wa kulelewa yeye na family na atabweteka,so kuepuka hilo kwangu kapuku ni big no,haijalishi hata nisipoolewa,my life my rules
Wanaume Tia maji ama pangu pakangu wanipitie mbali katika jina la Yesu
 
Na wewe naomba unijibu hilo swali
Mke akichepuka atakuwa ameji disqualify tayari, japo lazma ntaangalia chanzo. Kama ni makusudi au laa!

Kama amefanya hilo wakati hakuna tatizo baina yetu means amefanya makusudi. Then hapo ndio ita mark mwisho wa mahusiano yetu. Au ile mpo distant mda mrefu labda uko mkoa wa mbali lazma utakuta fisi wamempitia..hapo kitawaka.
 
Hapo ndipo dhana ya kiburi ilipojificha, kuna nyakati ambazo hata mshahara pia hucheleweshwa japo mmefanya kazi yenu tayari. Mbona hamuachi kazi kwa kiburi kwamba hamjalipwa?

Translation: Mume wako unahisi unammudu sana ndio maana unataka umuendeshe unavyotaka, ndoa sio kitu cha maana kwako.

Mume kukuhudumia ni swala mtambuka, lazma afanye hivyo ilihali ana uwezo sana. Ikiwa hana uwezo basi walau afanye yale yalio ndani ya uwezo wake na ukiona mumeo hakuhudumii kuna mambo mawili aidha hakupendi, au hana uwezo.
Unasema mume kama hamhudumii mkewe sababu mojawapo yaweza kuwa hampendi, really??kwanini uoe mtu usiyempenda??
Kwanini ujipe msalaba mzito hivo wanaume?
No wonder mnakufa kwa stress
Halafu mwanaume kutokuwa na uwezo ndilo alilosema mleta mada kuwa tafuteni wanawake wa viwango vyenu,kwani si kila sketi ipitayo ni size yako.
 
Zinayo sana,si ndo wanawake wenye elimu ndogo na wasiochangia lolote kwenye uchumi wa familia ambao wanaume ndo wanawataka
Lengo hasa ni kuwanyanyasa na kuwafuja,mtu hata hela ya kujinunulia lotion hana ataacha kupauka hahahah
Sio kweli
Ndoa hio haina raha at all kwa huyo mwanaume kwa kuwa ana mtreat mke kama substandard being..mapenzi gani mtu anaishi na mtu mzima mwenzake ili amcontroool? Mume hajiamini

Na mwanamke km huyo ana uchungu sana rohoni (from usaliti mume kuzaa nje,kutojaliwa,kutothaminiwa,dharau nk) na anarudisha the very same negative energy kwa mume mf hatoi unyumba,ananuna,hapendezi for the man, hana raha,kisirani hadi kwa watoto etc

Na mood ya mama ina reflect mood ya nyumba..ndoa km hio haina raha abadan kwa wote wawili

Ndoa lazma kuwe na dhana ya dhati ya upendo pande zote mbili na si element za woga za kumgandamiza mwingine
 
Zinayo sana,si ndo wanawake wenye elimu ndogo na wasiochangia lolote kwenye uchumi wa familia ambao wanaume ndo wanawataka
Lengo hasa ni kuwanyanyasa na kuwafuja,mtu hata hela ya kujinunulia lotion hana ataacha kupauka hahahah
Ndio maana kuna + na - mkuu, upo sahihi sana na hata hivyo kila mguu una namba yake, cha msingi ni uvumilivu ili upate namba yako.
 
Unasema mume kama hamhudumii mkewe sababu mojawapo yaweza kuwa hampendi, really??kwanini uoe mtu usiyempenda??
Kwanini ujipe msalaba mzito hivo wanaume?
No wonder mnakufa kwa stress
Halafu mwanaume kutokuwa na uwezo ndilo alilosema mleta mada kuwa tafuteni wanawake wa viwango vyenu,kwani si kila sketi ipitayo ni size yako.
Sasa kama mimi nakupenda na nina uwezo kwanini nisikufanyie yale mazuri kama mpenzi wangu, ona jana Diamond kanunua Land Cruisers mbili about 500+ millions. Moja ya mama yake na ingine ya mpenzi wake. Amefanya vile kwa sababu ana uwezo huo ila kwa sie tusio na uwezo tungefanyaje?

We would buy you a cake ukawasha na mshumaa sebleni tukakuimbia ikawa imetoka hio. Ndio liliopo ndani ya uwezo wetu. Doesn't mean haupendwi ila ndio kinachoweza kufanyika.

Huwezi kuolewa kama hupendwi ila unaweza ukafifisha upendo kwa tabia zako mbaya. Naweza kukuoa kwa moyo mmoja ila after 2 years nikawa sitaki hata kukaa nawewe japo for 2 hours maana ni kero tu.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
ndiyo ununue na private jet halafu ufanye kama Messi alivyofanya kwenye private jet yake kwenye zile ngazi za ndege yake kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini kaandika jina lake la mke wake na ya watoto wao watatu

tena nasikia ni mwanaume wa mwanamke mmoja yaani kama ambavyo kachezea timu moja tangu kaanza mpira ndivyo ambavyo kadumu na mwanamke mmoja na kazaa na mwanamke mmoja tangu kaanza mahusiano ila daah aise duniani kuna wanaume halafu kuna Messi
Jamaa ni kama mimi tu sema sichezi mpira tu. One girl attitude!!!
 
Back
Top Bottom