Mwanaume mipango robo!!!!!

Zahra White

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
598
Reaction score
576
Let me share my story with you guys.
Ilikuwa 2007 tulikutana katika social net iliyokuwa inabamba kipindi kile kwenye chatroom ya bongo5.
Alikuwa anaishi Turkey ni kijana wa kitanzania miaka yake 28.Mie ya kwangu ilikuwa 21.
Tukaanza private chat,tukahamia gmail na skype. Kutumia mapicha kwa sana nini kuongea kwa wingi.
Hakuniambia Turkey anajishughulisha na nini ila alisema kuwa anafanya vibarua na huku dar ataniunganisha na kaka yake anayemtumia hela kumjengea nyumba kama hekalu ya millioni 300.
Mtoto wa kike nikaona bwana nimepata chezea kuolewa na anayemiliki hekalu.
Its a dream for any girl. Jamani yule kijana tukawa karibu sana kila anachokifanya anajua na kila ninachokifanya anajua.
Akaniingia moyoni vibaya mwanaume yeyote akinitongoza namtolea nje chezea kuwa na boyfriend Turkey.
Mwaka ukaisha hilo hekalu linalojengwa sijaliona wala huyo kaka cjapewa mawasiliano yake.
Sikumuuliza siku akanipigia simu full unyonge full kulia eti alikuwa anamtumia hela kaka yake kujenga hekalu kaka yake kamdhurumu eti kiwanja kiko tu hata msingi hajaweka kachanganyikiwa nikambembeleza nikamwambia kuwa hela inatafutwa utapata nyingine ya billion moja.
Nikasema tobaaa hapa sasa hamna hekalu wala nini cha muhimu nianze kujiachia.
Kweli nikaanza mahusiano na watu tofauti tofauti .Born town mie mtoto wa Upanga maisha yakaenda jamaa mawasiliano yakapungua kasi.
Na mie nikashukuru nipate mda wa kuhanjam na wengine.
Ukiwa na mtaji mjini wanaume wanakuhonga mara 3 yake.
Nikatoka maskani upanga nikapanga masaki na mkoko juu hapo akuu mtoto wa kike chuo na mkoko.
Mie ndo mie nguo nikivaa sirudii a aaa nirudie waseme .... Kaniacha.
Sasa yule bwana mawasiliano yakawa kwa shida kwa mwaka mara 3.Mara akasema yupo dubai kweli code number za Dubai hapo mtoto wa kike nikawa napiga hesabu ya kwenda kutoa mkoko bandarini na kupokea magold na manguo kibao.
Mara kidogo simu akawa ananipigia rafiki yake mkenya anadai yeye hana simu.
Hata access ya internet hana eti niwe naongea na rafiki yake yupo mjini yeye yupo jangwani kwenye machimbo ya mafuta eti hawaruhusiwi simu.
Mweee dubai ndo dubai.
Mwaka juzi akanipigia simu kuwa anakuja hana pa kufikia,hataki kufikia kwa ndugu.Mie nikaona hapo ndo ulaji sasa atume hela nimtafutie nyumba he wakati nawaza hayo eti akaniuliza kama nimepanga afikie kwangu.
Nikaruka futi mia bado nakaa kwetu akasema hakuna possibility ya yeye kukaa kwetu.
Nikamjua no.Nikampigia bajeti ya chumba na sitting rum sababu alisema atakaa miezi 6 kisha ataenda Italy.
He he kumbe hata hela ya chumba kimoja hana.Akasema nakuja siku fulani nitafiki kwa rafiki yangu.
Mpítie rafiki yangu mje airport kunipokea.
Hapo hajui kuwa mwenzake nipo level nyingine kabisa.
Nikamuuliza rafiki yako ana usafiri akasema hana.
Ok nikamdanganya nitachukua usafiri wa nyumbani nitampitia kweli nikampitia rafiki yake tukampokea.Hapo nikasema labda hata kicheni kaniletea au baibui.
He nlipigwa na butwaa kidogo niwaache airport maana alikuwa na kifuko kiduchu ambacho hata tshirt haiingii.
Kwa mahesabu ya haraka nikasema hapo kaweka document muhimu tu kama passport,ticket n.k.
Kumanina nilijuta kuchoma mafuta from mbezi beach maana masaki nilishahama to Temeke then airport.
Nikawasha mchuma mpaka Temeke yeye mwenyewe alihisi kutetemeka alivoniona nimetokelezea kinoma classy&sexy,Very pretty akajua tu hapa mambo ya fedha yanahitajika kwa sana.
Basi mpaka temeke kwa rafiki yake.
Rafiki mwenyewe mchovu kinoma noma kapanga rum na sebule uswazi kinoma yaani kisebule kinanuka shombo.
Nikasema nini hiki akuuu shida sijazoea na sizijui nikailiza iphone yangu nikasingizia kuwa mama anahitaji gari.
 
Hahahaaah! Huna mawasiliano naye tena? Ulimuuliza japo kidogo nini kilimpata huko Dubai?
 
^^
Da! Nimeipenda
Inafundisha msipende wanaume wa Turkey
^^
 
Unatufundisha 2jue ulivyo malaya au

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Cyber love, huwa haiishi vituko. Sasa mipango yote ndio imekufa tena au utaendelea kumbeba?
 
yaonyesha itaendelea, wacha tumusubiri
 
what next mtoto wa upanga? Sasa kwa taarifa yako jamaa alituma mizigo yake kwa container, na hiyo ilikuwa kukupima kama kweli unampenda.
 
Huyu c ndo alisema ametembea na wanaume zaidi ya mia??,.......haya mama story teller endeleza story
 
hee naona kiswahili kimebadilika.kile cha mwanzo kimeishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…