Mwanaume kwenye mtongozo

Mwanaume kwenye mtongozo

Radium

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
490
Reaction score
871
Wakati naingia kucheki game ya uto fc na azam nikaangaza macho huku bin kule nijue pa kupoa.
Saa hiyo nshaeka oda jikoni na kuelekeza wapi muhudumu atanikuta(upande ulee).
Basi kuna kisu imekaa peke ake inapata some drinks nikaona wacha nione.
Nilikuwa nimevaa pensi na t-shirt ya bakabaka wa navy na kofia flani ya kitasha sana.

Mimi: Mambo. Hiki kiti kina mtu?(kwa kujiamini huku najikumbusha code ambazo nazivunja kila mara# eye contact #kifua mbele# mabega juu# sauti ya kuskika clearly)
Akajibu poa huku anatabasamu nkaeka tiki ya kwanza kwenye green lights
Yeye: "mmh huo uvaaji wako nimeukubali" huku ananiangalia kimapande (nkasema bingo)

Mimi🙁kwa sauti ya kukoroma huku nakaa kwa step) oh! Nlishasahau kuwa ndo nlizovaa. Ndo kwanza nimerud town.

Yeye: mh kutoka wapi?
Me: mikumi. Baada ya kupata kibali chetu cha uwindaji mbugani kwa taabu toka mwezi wa 11 mwaka jana.

Yeye: Hee. Si kuna wanayama wakutisha uko? Hamuogopi?
Me: Ni hatari na kunatisha ndio... ilaa hivyo ndo sisi wanaume halisi tunapenda kuishi maisha yetu.(uso mkavu)
Sas utasemaje nikikuelezea nilivyoenda kwenye uvuvi wa jadi maeneo ya mto wa Congo katikati ya misitu yao.?
(Wakati anashangaa shangaa)
Nikikueleza nilivyo kimbizwa na bonge la nguruwe pori nikiwa na jamaa angu aliyekuwa na mguu mbovu mpaka nikamuua huyo nguruwe kwa mikono yangu?

Yeye:

Mimi: Unajua changamoto nliyopata mpaka namjengea mama yangu nyumba nzima...... KWA MIKONO YANGU.

yeye: daah.

Nikaona hapa nikizidisha chenga ntautoa nje.

Mimi: Hatari ndiyo humjazilisha MWANAUME wa kweli, sio wanawake wengi au pesa.

Yeye: (Akaanza kujitia wakileo eti) Unajua masculinity sku hizi imekuwa kitu adimu sana watu wamekopi umagharibi na mambo ya muvies.

Mimi: Huyu mwanaume halisi... angependa kuchukua namba ya mrembo huyu(huku navuta ng'ora)

Akaanza kutype pale huku nimeeka mikono yangu mezani kama mtasha.

Palepale muhudumu akaniletea chipsi na juisi ya embe ya U- fresh. Ile anataka kuniekea pilipili akaambia na jamaa wa jikoni "hatumii pilipili huyo"

Kwa kifupi namba nliyopata ni 07 basi nikarudishiwa simu kwa kuchekwa.

#Mwenye vitafunwa mchana huu alete
 
Nna kichwa kigumu kuelewa au hapo mwishoni ndio hapaeleweki.?
Aliandika namba mbili tu (07) ikaishia hapo baada ya kuona chips na U fresh juice?
Au alikupa mtandao pendwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom