Mwanaume, kuoa mke anaye kuzidi elimu/mshahara

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,756
Reaction score
2,309
Habari wapendwa, hebu tuzungumzie hii kitu kidogo najua kuna Magreat thinkers kibao humu ndani!
"Wahenga walisema Mapenzi hayachagui pesa Wala elimu" Huu msemo some time naweza sema ni msemo ambao tumekuwa hatuutendei haki baadhi yetu!

Lakini Je kwa upande mwingine, Kuwa na mpenzi au mke anaekuzidi elimu, kwa mfano: Mwanaume una Cetificate ya chuo au Form 4 failure, na yeye ana Degree au Masters, Kipato chenu kinatofautiana sana we unalipwa laki tano ye analipwa Milion na point kazini kwake,

Sasa kwa uhalisia wa maisha yetu ya leo inaweza kuwa na madhara na kufanya mke huyu akushushe heshima kiasi kwamba heshima itapungua ndani kwa kummiliki vizuri kama mke?

Huku mtaani huwa tunapolizungumzia hili swala watu wengi huwa wanaseme haiwezi kutokea akaoa mkea anae mzidi elimu hata kidogo.

Wanaume wenzangu ebu tubadilishane idea Hii inaweza kuwa kikwazo katika mapenzi!

____NAWASILISHA HOJA____
 
Wakati wa kufunga ndoa mnaapa kuvumiliana wakati wa shida na raha. Kazi na mishahara ni vitu vya mpito tu. Kikubwa cha kujiuliza je ntaweza kumvumilia mwenzangu kwenye shida na raha?
 
kabisa Kiongozi
 
Wanawake wanakubali kuvumilia ndani ya shida na raha lakini baadae hugeuka maana huwa hawana msimamo na wengine wanadanganywa na wenye kipato kikubwa yaani majiri kwa namna moja ama nyingine.
 
Inaonesha ulivyo mwoga. Sasa akina Makinda wao hawana waume au? Akina Silima, kina Joyce Banda we vipi?? Siendi kuoa elimu au kipato chake. Namwoa mwanamke wa kike sio wa vijisenti vyake. Akiingia home, tunapangiana majukumu, kama zake ndo nyingi anaziweka mezani nazipigia mipango elekezi kama kichwa cha nyumba na yeye anasema ndiyo baba. Yawezekana nilimwoa akiwa mwalim wa Pr. School. Cheo kakipatia kwangu tukiwa na watoto 10. Nimwache??
Anaenda Ulaya na Marekani kwenye vikao vya Wakubwa wenzake nami nimo namngoja hotelini au naenda shoping. Kwani nini, nyie semeni mi ndo naijua nyumba yangu. Ukimwogopa ati kwa sababu ni Rais, ni rais wetu sote lakini kwangu jioni ni mke wangu aliye mwanamke tu tunaye pendana si rais. Nisameheni kina mama nilo wataja kwani ndio mfano mzuri.
 
Ndoa ni UAMUZI na watu wawili wawe wameamua kukubalina jinsi walivyo. Ikiwa mtaoana kwa kufuata hisia zetu, UHALISIA utawaumbua huko muendako.

Sioni shida kama mwanamke amekukubali ulivyo nawe umemkubali na mkachukuliana mlivyo. Tatizo ni hili.. HELA INALETA KIBURI NA KUJIINUA NA BAHATI MBAYA WATU WENGI HAWAJAWEZA KUISHINDA HII TABIA HADI LEO. KWA HIYO HUENDA MTU AKAWA NA NIA NJEMA KABISA LAKINI AKASHINDWA KUWA NA TABIA ZA KUISHINDA NGUVU YA PESA YAKE. Hivyo kuishia kumnyanyasa mwenzake.

TUNAPASWA KUITAWALA PESA/MALI. KAMA BADO UNAITETEMEKEA PESA. POLE YAKO.

Habari wapendwa, hebu tuzungumzie hii kitu kidogo najua kuna Magreat thinkers kibao humu ndani!
"Wahenga walisema Mapenzi hayachagui pesa Wala elimu" Huu msemo some time naweza sema ni msemo ambao tumekuwa hatuutendei haki baadhi yetu!

Lakini Je kwa upande mwingine, Kuwa na mpenzi au mke anaekuzidi elimu, kwa mfano: Mwanaume una Cetificate ya chuo au Form 4 failure, na yeye ana Degree au Masters, Kipato chenu kinatofautiana sana we unalipwa laki tano ye analipwa Milion na point kazini kwake,

Sasa kwa uhalisia wa maisha yetu ya leo inaweza kuwa na madhara na kufanya mke huyu akushushe heshima kiasi kwamba heshima itapungua ndani kwa kummiliki vizuri kama mke?

Huku mtaani huwa tunapolizungumzia hili swala watu wengi huwa wanaseme haiwezi kutokea akaoa mkea anae mzidi elimu hata kidogo.

Wanaume wenzangu ebu tubadilishane idea Hii inaweza kuwa kikwazo katika mapenzi!

____NAWASILISHA HOJA____
 
Age is just a numeral tu dude... kamata kiuno, tupa kule, ndoa yako itadumu miaka 200!
 
Mwanaume atakua kichwa na mwanamke ni msaidizi

Kua kichwa hakuji hivihivi means awe provider mkuu na in-charge wa kila kitu kinachohusu familia,wakati huo mwanamke anampa support ya hapa na pale (Ikiwa vice-versa ina maana ke ndio provider na me' ni msaidizi huko ni kuidhalilisha nature ya kiumeni)

Kama mwanamke kakuzidi elimu jitahidi asikuzidi na kipato

Kwa huo mshahara wako wa laki 5 itabidi ujiongeze kwenye vijibiashara to earn the so called respect na kueza kwenda sawa!!
 
Habari wapendwa, hebu tuzungumzie hii kitu kidogo najua kuna Magreat thinkers kibao humu ndani!
"Wahenga walisema Mapenzi hayachagui pesa Wala elimu" Huu msemo some time naweza sema ni msemo ambao tumekuwa hatuutendei haki baadhi yetu!

Lakini Je kwa upande mwingine, Kuwa na mpenzi au mke anaekuzidi elimu, kwa mfano: Mwanaume una Cetificate ya chuo au Form 4 failure, na yeye ana Degree au Masters, Kipato chenu kinatofautiana sana we unalipwa laki tano ye analipwa Milion na point kazini kwake,

Sasa kwa uhalisia wa maisha yetu ya leo inaweza kuwa na madhara na kufanya mke huyu akushushe heshima kiasi kwamba heshima itapungua ndani kwa kummiliki vizuri kama mke?

Huku mtaani huwa tunapolizungumzia hili swala watu wengi huwa wanaseme haiwezi kutokea akaoa mkea anae mzidi elimu hata kidogo.

Wanaume wenzangu ebu tubadilishane idea Hii inaweza kuwa kikwazo katika mapenzi!

____NAWASILISHA HOJA____

aaaaaah wapi, mume ni kichwa na itabaki hivyo irrespective of mshahara, elimu na cheo cha mwanamke, mbona kuna jamaa hana kazi kabisa na anaishi na mkewe ambaye ni mwajiriwa

ni kujitambua tu
 
Umenifurahisha...unaona Rais; wakati yuko kwenye kikao na Obama wewe unatembelea designer shops tuuuuu....Mungu akupe nini? Kidonda ndugu...

waache hawa kina sizitaki mbichi hizi....maana si kila mtu mwenye bahati ya kupata mke mambo swafi te te te

Ndoa itadumu si kwa sababu ya pesa or lack of it...ila kama umeoa mpenzi na rafiki yako...

Inaonesha ulivyo mwoga. Sasa akina Makinda wao hawana waume au? Akina Silima, kina Joyce Banda we vipi?? Siendi kuoa elimu au kipato chake. Namwoa mwanamke wa kike sio wa vijisenti vyake. Akiingia home, tunapangiana majukumu, kama zake ndo nyingi anaziweka mezani nazipigia mipango elekezi kama kichwa cha nyumba na yeye anasema ndiyo baba. Yawezekana nilimwoa akiwa mwalim wa Pr. School. Cheo kakipatia kwangu tukiwa na watoto 10. Nimwache??
Anaenda Ulaya na Marekani kwenye vikao vya Wakubwa wenzake nami nimo namngoja hotelini au naenda shoping. Kwani nini, nyie semeni mi ndo naijua nyumba yangu. Ukimwogopa ati kwa sababu ni Rais, ni rais wetu sote lakini kwangu jioni ni mke wangu aliye mwanamke tu tunaye pendana si rais. Nisameheni kina mama nilo wataja kwani ndio mfano mzuri.
 
kikubwa ni mapenzi ya dhati. mkipendana kweli hautaona hizo tofauti.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom