Mwanaume kulia si udhaifu, kuna faida kiafya ukulia

indelible

JF-Expert Member
May 2, 2015
652
299
Za leo,

1. Ebu tujuzane nini taswira inayo patikana mwanaume unapolia mbele ya mkeo, mpenzi au mchumba wanawake huwa mnachukiliaje?

2. Kwa wanaume hii huwa inasababishwa na nini? (Achialia mbali uliaji wa maafa mfano kufiwa au majanga ya kiasili) ni kwamba unajaribu kuteka hisia au utafuta huruma au?

3. Sikuongelea wanawake maana ni kitu kama kilichozoeleka hivi.

Nimeandika hivi baada ya bwana mmoja kuangua kilio mbele ya girlfriand wake akihisi eti gf wake kamcheat yaani kaangua kilio cha haja huku akitamka "ulikua na mwanaume jana siku nzima ulizima simu".

Maoni yenu

======



Wataalamu wa afya wanadai kulia kwa kutoa machozi kuna faida kiafya kama kuondoa bakteria wa maambukizi machoni & kuondoa mkazo (stress), wasiwasi (anxiety) na huzuni. Kulia pia si udhaifu, ukijizuia kulia ni kama kuhifadhi moto moyoni wakati wowote utakuchoma.

Wataalamu wanaamini kulia ni njia nzuri ya kutoa yaliyo moyoni na tukizoea kuepuka kulia tunaweza kudhuru afya zetu. Wengine wanabisha, wakidai kwamba faida za kimwili au za kiakili za kulia bado hazijathibitishwa kisayansi. Hata hivyo, utafiti unaonyesha kwamba asilimia 85 ya wanawake na asilimia 73 ya wanaume huhisi vizuri baada ya kulia.

Aina Tatu za Machozi
  • Machozi ya Msingi. Tezi za machozi hutengeneza umajimaji huu ambao hulowanisha na kulinda macho yetu. Pia, huboresha jinsi tunavyoona. Tunapopepesa kope za macho, majimaji hayo husambazwa machoni.

  • Machozi ya Ghafula. Machozi haya hufurika unapoingiwa na kitu kinachokera machoni. Machozi ya ghafula hutoka pia kwa sababu ya vitendo fulani, kama vile kupiga miayo na kucheka.

  • Machozi ya Hisia. Haya ni machozi ambayo binadamu hutoa ili kuonyesha hisia nzito. Machozi hayo yana asilimia 24 zaidi ya protini kuliko machozi ya ghafula.
Imezoeleka wanawake ndio ambao hulia wakishikwa na uchungu au maumivu ya kihisia.

Na kuonekana ni jambo la aibu au udhaifu kwa mwanaume kutoa machozi pale anapolia hata kama kaumizwa basi hutakiwa kuvumilia na kulilia moyoni.

Jambo hili limepelekea wanaume wengi kuishi na uchungu moyoni na kuwa wagumu wa kuachilia mambo kwa kuwa moja ya njia ya kumaliza uchungu ni kulia na kutoa machizi, na wao hawafanyi hivyo.

Faida za kulia

1. Kusafisha macho.

Unapolia, machozi hutoka na baadhi ya uchafu uliokuwa ndani ya macho ikiwa ni pamoja na vumbi.

2. kutoa uchungu moyoni.
Kulia kunapunguza uchungu wa mambo au jambo ambalo linakuwa limekuumiza kihisia na kufanya ubaki huru.

3. Kuonesha hisia zako.
Mtu anapolia huonesha hisia za kwamba ameumizwa na kuweza kupatiwa msaada iwapo unahitajika.

Michango ya wadau:

----
----
 
Binadaamu wako tofauti

kuna wengine wanalia kiusanii tu kumshawishi mwanamke 'wamefika'

wengine wanalia wakiwa na hasira kupita kiasi

wengine wanalia kwa unyonge.....

wengine wanalia kumhadaa mtu
Hahahaa hiyo kiusanii kwamba wmefika ikoje hiyo?
 
Unamtazamo ila cjajua kama ni kweli

Kama unaweza ukalia ukiwa peke yako, that means mwanamke ndo anakufanya usilie mbele yake.

Inaonyesha hujiamini, na kinachokufanya uwe naye ni huko kutolia mbale yake. Kumbuka wengine mitazamo yao juu ya uanaume ni mojawapo ya haya au combination ya kadhaa;

1. Kufungwa magerezo magumu
2. Kuhakikisha anatimiza majukumu yake iopasavyo
3. Kutokulia mbele ya wengine
4. Kupigana na wengine huku akionwa na mwanamke wake
5. Chapa vibao, makofi mangumi mateke mwanamke wake
6. ....

etc.
 
She has seen you naked, with your funny looking asian inherited lil man, and she's still down, what's tears?? Wanna let out your anger, frustrations or whatever, just let it out man. It's ok to be your woman's 'b!tch' for a few seconds.
 
We binafsi huwa unachukuliaje mwanaume akilia mbele yako...kama imewahi kukutokea

Imewahi, everyone has their weak moments, ni jukumu la huyu anaeona kumsaidia mwnzake kimawazo,cz mtu yoyote hadi alie ni ktu kimemsukuma kufanya hvyo..mi binafsi sijazoea kuona mwanaume akilia.

So nilivyoona i was like oh!duh and found a way to comfort tht person....ila mwanamke bwana, mxa mwanaume akilia th first thng it just touches her heart, kihuruma fulani kinakuja kumbe wengne feki tu hahahaaa
 
Ni kawaida yangu kutojisikia/kutaka kulia wala kutapika.Kwa ufupi sijawahi kulia mbele ya mwanamke au mtu yeyote,naamini tangu nihame umri wa utoto.

Ingawa kitabibu tunashauriwa ujisikiapo kulia,wewe lia ili upunguze hasira/ sumu mwilini kwa afya ya mwili na akili.
 
Aafuu wengine wakililiwa tu wanagegedwa huku wanalia wao... Yaani kilio kinahamia kwake
 
Daaaaaaaaa kulia kwa hasira ishawahi nitokeaa nilipomfumania dem wangu nilitaman kuua lkn mungu akanisaidia yakapita.ss npoo nasubiri kujiandikisha kumchagua rais nimtakae
 

Kwa hiyo wewe misumu yako na mahasira vyote vimekujaa mwilini....

Ahahahahahaahaa ndo maana wengine wakijammba vinanuka hatariiii... kumbe tunanusishwa na sumu ... DUH, SUMU, HATARII
... embu lieni tupunguze harufu mitaani
 
Binadaamu wako tofauti

kuna wengine wanalia kiusanii tu kumshawishi mwanamke 'wamefika'

wengine wanalia wakiwa na hasira kupita kiasi

wengine wanalia kwa unyonge.....

wengine wanalia kumhadaa mtu

Enzi hizo tunakuwa kulikuwa na jamaa mmoja bingwa wa kuimbisha mademu kitaa! Silaha yake ya mwisho ni chozi! Demu lazima alegee tu kwa kuamini jamaa kapenda saaana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…