Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,512
NOTE:
Hii haiwahusu wazinzi.
Kuna baadhi ya wanaume wenzangu wanaogopa kuoa wanawake warembo kwa kuhofia kuwa eti wanaweza kuibiwa hivyo huona kuwa mwanamke wa kawaida ambao wao huwapa sifa ya wife material kwa maana hawana gharama na ni watulivu.
Watu wanaweza kuwa na madai yanayoonekana kuwa na mashiko kwao ila yakawa hayarandani na tabia halisi walizonazo wengine ambao kiukweli unakuta wametoka kwenye malezi tofauti.
Kuna watu wanakariri kuwa mwanamke/mwanaume wa kabila fulani wako hivi hivyo si wa kuoa, wanashauriana owa wa kabila fulani ndio watulivu nk.
Kwanza kama wewe sio mtulivu mwanamke atakuwaje mtulivu? sote tumepitia shule ambapo unakuta mtoto anakuwa mtukutu ila kwa uthibiti wa mwalimu mwanafunzi anabadilika na mwalimu akiwa mzembe atadharauliwa, mfano huo ni halisi kwenye maisha ya ndoa kwamba mwanamke/mwanaume unamjenga wewe na ukisubiri au ukiacha mambo yaende yenyewe kama yalivyo utaishia kudharauliwa na ndio utakuwa mwanzo wa kuchapiwa na wanaume wenzako.
Mazingira yanayokuzunguka(mahali ulipo mara kwa mara)ndio yanaumba tabia yako na mwenza wako na ndipo utakapopata marafiki huko.
Kama unadhani kwenda kunywa bar na mke wako ni ujanja nenda maana utamzoesha hivyo na hata siku ukiwa haupo ataenda kwa kuwa tu unaridhia mazingira hayo na hapo hapo ndipo atapatikana mbaya wa ndoa yako, kwanini usibadilike? mambo mengi mnayoyafanya kihisia ndio yanawagharimu baadaye.
Unaacha rafiki zako wazoeane na mkeo kwa kuwa tu wanamwita shemeji, siku ukiwa mbali kikazi juwa umeliwa maana wakienda nyumbani kwako hata majirani hawatakuwa na hofu na hata mke wako hatakuwa na wasiwasi kwako kwa kuwa ukiwepo wanakuja na hata usipokuwepo watakuja tu kwa kuwa ni rafiki zako.
Unaacha kumhudumia mke wako mahitaji mbalimbali muhimu unategemea nini?
Ngoja nikuambie.Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi wanaokuletea matatizo baadae ni wale ulionao karibu na ambao umewaamini sana kwa maana ya marafiki na mwisho wake ni kuumizwa tu.
Unapoingia hatua ya maisha mapya ya ndoa au hata uchumba wa wazi hakikisha unabadili maisha yako kiujumla, kama ulikuwa unaenda kwenye kumbi za burudani acha mara moja, tabia hiyo itakugharimu baadae.
Mwanamke sio ndugu yako, hakikisha hakuzoei na kila siku akuone wewe ni mtu mpya, mpende na umjali ila asikuzoee na usipende kuweka wazi mambo yako yasiyo na ulazima kwa mwanamke maana atakuchoka mapema, na hapa ndipo watu wanajiuliza ni kwanini wakati wa uchumba ni tofauti na kipindi kifupi baada ya ndoa kuanza?
Kama kuna mitoko ya kifamilia hakikisha mnafanya mitoko kwenye sehemu maalum tu na mara moja moja sana kama kutembelea hifadhi za wanyama, sehemu za kihistoria kama bagamoyo nk na hakikisha unaambana na mkeo au ndugu zake/zako tu, waache marafiki zako nao wawe na safari zao na wake zao.
Ukiwa mcheza disko hata kama mke wako ni mshika dini mzuri sana polepole atabadilika na kuwa kama wewe, kwanini usibadilike sasa?Unaacha mke wako avae nguo zinazoacha mwili wake wazi unataka wanaume wenzako waone halafu wafanye nini?
Unafanya mazoea makubwa nyumbani kwako na watu unaoishi nao karibu, wakikujua tabia yako na madhaifu yako ya nyumbani kwako watakudharau na ndio mwanzo wa kukuona kuwa hata wakitoka na mke wako huna cha kuwafanya(mazoeano ni huko nje sio kwako).
Ni mara ngapi unajikuta unamtamani mke wa mwenzako ila ukijua aina ya mwanaume aliye naye unaghairi mipango yako? unadhani ni kwanini?
Usipoziba nyufa utajenga kuta
Maji hufuata mkondo.
Ukipanda mahindi utavuna mahindi.
Ndege wafananao huruka pamoja
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
Penye mzoga ndipo wakutanikapo tai
Rafiki yako ndio adui yako
Penye miti hakuna wajenzi
Haba na haba hujaza kibaba
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE