Mwanaume kubeba mimba

Hiyo ni ndoto tu mkuu kama unavoweza kuota upo na yesu unamzuia asitende maovu
 
Ila mwisho wa siku ktk comments 100, kuna comments kama 30 au 40 unakuta mleta mada anakuwa kapewa jibu angalau akaridhika. Yaani comments za ile jf yenyewe.
 
Ulishawahi kwenda kwa waganga wa kienyeji kabla ya Ndoto hizo? Tuanzie hapo ukijibu kuna majibu
 
Jf umejawa na watoto wadogo mno saivi hasa nyakati hizi,
Watu wanakosa maarifa kabisa.mleta madam yuko seriously lakini comment za ajabu ajabu duh!
Pia tatizo ni mods kuwa watoto watoto.
Sijui nitapigwa ban hapa!
 
Ndoto ni maono ya mambo yaliyopita, yaliopo na yatakayokuja. Ndoto huweza kuakisi mawazo,i mtizamo, falsafa, mitindo ya maisha ya mhusika. Pia huweza kuwa matokeo na dalili ya ugonjwa fulani uliomo mwilini, kula chakula kingi kupita kiasi, kulala sehemu isiyo rafiki na kuwa na mkojo mwingi kwenye kibofu.

Ndoto ni mawasiliano baina ya roho na mwili, ndio kitu pekee ambacho kinauunganisha nafsi, mwili na roho.

Si kawaida ndoto kujirudia, na hii ikitokea basi lazima kunataarifa ya msingi inatolewa na ndoto husika.

Kulingana na ndoto yako, lazima uwe na wasi wasi kwani si kawaida kwa mtu wa jinsia kama yako kuota kitu kama hicho.
Umesema umeota unaujauzito ambao ni mapacha.

je unakumbuka ulikuwa na nguo za rangi ipi?
je ni nguo za kiume au za kike?
Ulipofika Leba, je wauguzi walikuwa wangapi na wamevaa nguo gani?
Je, walikuwa wa jinsia moja?
Ulipokuwa unashikwa tumbo wauguzi walisimama katika nafasi(position) zipi?
Unakumbuka lugha iliyotumika?
Unaweza hisi mazingira ya tukio?
Je kuna tofauti yoyote ya ndoto ya kwanza na ya pili?
Kama jibu ni "ndio" taja tofauti hizo

Je umeoa/hujaolewa?
Je unamchumba/mpenzi?
kwenu mmezaliwa wanaume na wanawake wangapi?

Mambo ya kufanya:
1.Epuka kukaa mwenyewe na kuangalia picha zisizofaa
2. Epuka kulala ukiwa umepaka marashi, manukato,mafuta na vitu vyovyote vya kunukia
3. Sali,omba, au piga dua kuomba ulinzi wakati ulalapo
4. Epuka mawazo yanayokinzana na jinsia yako

Ni jibu alafu tuone nini tatizo.
 
Wahi clinic mapema
 
ndoto za majini hizi! nenda kaokoke! doto za majini zikiambatana na roho za kishoga!
 
Hiyo ni ishara ya utajiri wa maajabu jiandae na ongeza juhudi kwenye kazi zako
 
Sikumbuki nimevaa nguo gani
Nilikuwa nimevaa nguo za kiume
Nilimuona mama mmoja tu akiwa amejifunga kanga kwenye maziwa mama mnene sana
Sikushikwa tumbo bali nililishika mwenyewe
Lugha iliyotumika ni kiswahili
Tofauti ya mazingira kiukweli sikumbuki vzri kwa ndoto ya kwanza Ila hii ya pili nilihis hilo tukio nikiwa njian natembea nikiwa na mdada ambaye simjui lakini nilienda naye mpka wodini
 
Sijaoa Ila ninampenzi
 

ndoto ya kwanza uliota mwaka gani?
unamiaka mingapi na mpnz wako?
wodini ulivaa suruali au bukta?
 
Kaka tumelelewa tofouti sehemu mbalimbali...... kwangu ata mke angu siwezi kumsimlia ndoto kama hiyo naka nayo mpaka nakufa nao.... kwetu mwana ume ni mwana ume tu
 
Kiimani....
Kuna mzigo wa dhambi mkuubwa saana unao, na Mungu anakukumbusha kua utubu.
Omba saana sali sana kwa iman yako ukitubu kwa kulia hutoota tena ndoto hiyo na kemea pia.
 
Pole sana Mkuu ushauri Zaidi muone kiongozi wa dini umuueleze pia mwombe Mungu saba
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…