Hapana, watoto hawafi, kwani hata ukikaa huna msaada, refer vizuri uzi, umekosa namna yeyote ya kuingiza chochote. Bora usepe ukapambane kiume, Ukipata hata buku unamrushia mkeo, awanunulie dagaa.
Ukiendelea kubaki hapo, watoto watashuhudia udhalilishaji, majibizano makali, na hata kupigana, kitu ambacho kitawaathiri kisaikolojia. Hii nazungumzia kwa mwanamke mjeuri, asiye na adabu na ambae hawezi kuvumilia kwenye nyakati za shida, ambao ndio wengi siku hizi.