Hivi jamani inakuwaje sikuhizi vijana wengi kupenda mabinti walioajiriwa? Mara nyingi vijana hawa shule ni ndogo na wanawadanganyika mabinti kuwa wanafanya na kumiliki biashara kubwa zinazowaingizia kipato wakati sio kweli. Muda mwinigi hushinda kijiweni. wakisha wapata mabinti hao basi wao ni kula kulala. binti aende kazini yeye yupo tu nyumbani. tabia mabay walionayo ni ku-divert namba za simu za wapenzi wao ili wafahmu wameongea nani siku, wanaiba PASSWORD za email za wapenzi wao, na PIN namba za ATM. wanawashawishi waombe mikopo kwenye mabenki ili wafanye biashara, lakini fedha hiyo huishia kufanyia starehe. Kama hiyo haitoshi wanawazuia wapenzi wao kutosaidia ndugu zao hata wadogo zao utadhani pesa ni zao au wao ndio waliwasomesha. matokeo yake ni mabintihawa kuishi maisha ya utumwa wa mapenzi kwa kuwatumikia manaume/ au wapenzi wao.hivi huu kweli ni uungwana?
mmmh, nadhani kama ulivyo sema tatizo ni shule na akili, na nadhani huyo binti nae atakaekuwa anatazwa kusaidia ndugu zake au kurubuniwa na mvulana wa namna hiyo nae atakuwa ana matatizo ya akili pia.
Mwanamme wa kijiweni wa nini? atawafundisha nini watoto zaidi ya uzembe,ah babu wee mwanamme kazi japo awe na mshahara mdogo.lakini asubuhi mke anakwenda kazini mume umelala huna baisha nzuri wala mbaya mzigo wa nini bora ule yatima kuliko mashaka hayo...
mtu hata ukiwa in so called ''love'' lazima uwe na akili ya ziada..yani mtu ashinde kijiweni nimpeleke wapi..nitaanzaje kuchukua mkopo kwa ajili ya mwanaume tustarehe??
Hao mabinti wa kiume sina mcheche nao kabisa. Mwanaume kuwajibika hata kama ni ''good for now'' type..