Mwanaume jina nimfanyeje?

uajekundu

JF-Expert Member
Jan 14, 2016
541
461
Habari zenu wana jamvi, kuna kisa kinanichanganya naombeni ushauri wenu.

Kuna rafiki yangu amekua na boyfrend huu ni mwaka wa 9 ni tangu wako chuo shule. Walivyomaliza shule mdada akapata kazi nzuri tu na mkaka amekaa sana kitaa ila kwa sasa amepata kazi wizara moja serikalini.

Tofauti iliyopo ni huyu dada ana hela nyingi sana kumpita mkaka, mdada ana gari ni mwaka wa tatu huu lakini mkaka bado anaswampa kwa miguu.

Tatizo ni huyu kaka amekua haoneshi dira yoyoye ya uhusiano wao. Mdada amedai ndoa mpaka amechoka.

Miezi mi4 au 5 iliyopita mdada akapata ujauzito mkaka hayuko tayari kwenda kujitambulisha kwa kina mdada wala kumtambulisha mchumba kwao.

Haoneshi dalili zozote za kutaka kuachana, ila inapokuja suala la ndoa hasemi kitu, wanaweza wakapanga siku ikifika mkaka anakua busy.

Toka mdada apate mimba mkaka hajawai kuchangia hata sh.10 ya matunda kwa mdada tho mdada anajiweza haitaji hela.

Suala inakuja pale mdada haelewi je aachane na huyu mkaka asonge na maisha yake au aendelee kumsubiria siku asiyoijua?

Au amlazimishe kumuoa kwa nguvu? Amvute kumpeleka kwao? Ndoto za mkaka ni kununua gari na vitu vidogo vidogo but sio kua na familia coz haoneshi utayari wowote.

Umri wao ni miaka 27 kwa 29 mkaka.

Ushauri wenu wakuu
 
WABABA TUNASEMA........

1. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo." *Napoleon_Bonaparte.*

2. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake." *George_Patton.*

3. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa." *John_Adams.*

4. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi." *Sun_Tzu.*

5. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda." *Harry_Browne.*

6. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso." *Adolf_Hitler.*

7. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea." *Friedrich_Nietzsche*

8. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka." *Confucus*

9. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo." *Albert_Einstein.*

10. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote." *Plato.*

11. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo." *Harry_Truman*

12. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili." *Benjamin_Franklin*

13. "Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria" *Lamar_Smith*

14. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa" *Doug_Larson*

15. "Siasa ni hatari kuliko vita. Kwenye vita mtu hufa mara moja tu, lakini kwenye siasa mtu hufa na kufufuka mara nyingi kadri iwezekanavyo" *WinstonChurchi
 
umemuuliza rafiki yako sababu kubwa ya kukimbilia ndoa.... au amepata tetesi nje...!!!!
 
Nipatie namba ya huyo rafiki yako mimi napendaga sana wadada kama hao nakuhakikishia hatalia lia tena ovyo
 
Hahahaha, kaasilika kisaikolojia kutokana na kusugua benchi Sana kitaani baada ya kuhitimu, mvumilie atakaa Sawa tu mda so mrefu baada ya kupata hiyo kazi
 
Kama ulivyosema hapo awali hao ni MDADA na MKAKA hakuna ndoa hapo, mkaka anaosha rungu Ilan mpango wa kuoa hana, mwambie MDADA ajiunge na JF huku wapo watu wanatafuta wenzao was dizaini ya MDADA hatojuta...kila la kheri.
 
anyways, hapo huyo Dada kama vipi mwambie ajiongeze tu ataakaje na Msela asie jishughulisha..?? Na huyo rafiki yako mwambie pia aache mambo ya ajabu aseeh ajishughulishe alee mimbaa hiyo
 
Hilo ndio kosa ambalo wanawake tulio wengi huwa tunalifanya. Kujitegesha hadi kupata mimba hilo tayari ni kosa ameshafanya hasa kwa mtu ambaye hakuwa na muelekeo.

Pia hakuna kilichoharibika kwa kuwa uwezo anao alee hiyo mimba mwisho wa siku ajizalie mwanae. Hakuna haja ya kuendelea kuumiza kichwa kwa mtu asiye na muelekeo.
 
miaka 27 kwa 29. tatizo linaanzia hapo, uwezo wa kufikiri na kupambanua wa mwanamke ni mkubwa kuliko huyo mwanaume hana sababu ya kulazimisha ndoa atulie azae baada ya miaka 3 akajiweke kwa muhenga wa miaka 37 mwenye mtoto walee watoto wao kwa pamoja huyo mvulana wake kadata kwa kabinti ka miaka 20 maana hasa ndio wanaendana ila sio huyo rafiki yako wa miaka 27
 
Kwasababu umri umefika na amenasa ujauzito...uhusiano wa kiboyfrend zaidi ya miaka 9 sio issue
 
Hizo pesa alizonazo huyo rafiki yako pengine ndio sababu ya huyo jamaa kuwa mzito wa kufanya maamuzi. Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa huenda kuna manyanyaso makubwa sana anayapata kutoka kwa huyo dada au kuna vijitabia vya jeuri na kiburi cha fedha kinachofanywa na huyo dada ukizingatia huyo jamaa hayuko vzr sana mfukoni. Kitu ambacho wadada wengi wanashindwa kuelewa ni kuwa mwanaume anahitaji kupewa heshima kama mume haijalishi hali aliyonayo.

Ushauri:
Huyo rafiki yako ajichunguze kwanza kabla hajaanza kutupa lawama kwa jamaa yake, pengine kuna mambo anakosea na jamaa anahisi akiingia kwenye ndoa yatamsumbua zaidi.
Ikishindikana hapo basi atumie akili ya kuzaliwa na aachane na harakati za kubisha hodi ukutani akitegemea mlango kufunguka.
NB: Wanaume wapo wengi.
 
Wanawake watu WA ajabu Sana.

Unakuta anamwacha Jamaa mzuri anamfuata Jamaa WA ovyo kabisa yaani Hawa watu wana upofu WA akili

Hapa nilipo kuna kisa Kama hiki mdada kajiajiriwa serikalini halmashauri Fulani ana miaka Kati ya27-29 kazi nzuri kazalishwa na dogo tu WA miaka 20 aliekimbia shule na Hana mchongo wowote WA maana Kitaa .

Yaani nyie hata wasome vipi lakini kuna insanity part inawalet down daaah so sad
 
Mi naona uyo kaka anataka awe stable kwanza kimaisha ndo aoe ni wale aina ya wanaume wasiopenda wawe na wanawake waliowazd kipato asifanye kosa la kumlazimisha mwanaume kuoa coz ata akiolewa kama mwanaume hajapenda ata ndoa ataiona chungu mwanaume anatakiwa apropose mwenyew
 
Usitegeshe mimba kwa mwanaume asiye na malengo kwa kuwa tu jamaa ana uwezo au ili kuongeza Upendo.
Siku hizi wakaka hawabustiwi kwa mimba.
Ukitega mimba ndiyo kwanza anakukimbia.

Mbona kuna vitu vingi vya kumpima mwanaume kama anakupenda? Hapo ndipo mnapo haribu madada.

Tatizo linalokuja baina ya wapenzi;
Upendo unazidi kipimo cha akili.
 
Kuna watu wavumilivu yani miaka yote hiyo haonyeshi malengo na mimba unabeba hahaha lol wanawake vingine tunajitajia tu.
 
Back
Top Bottom