Mwanaume hupaswi kuoa mwanamke mwenye mtoto kabisa

Pi Network

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
290
319
Mwanaume yeyote anayeelewa maana halisi kabisa ya kuoa, hapaswi kuthubutu kumuoa mwanamke ambae tayari ana mtoto hata kama mtoto huyo alimpata kwa bahati mbaya. Labda kama mzazi mwenzake ameshafariki, vinginevyo usijaribu.

Elewa kwamba, kumuoa wewe hakutoweza kuvunja uhusiano/mawasiliano yake na mzazi mwenzie. Mara nyingi mwanamke aliyezaa na mwanaume fulani anapofikia uamuzi wa kuolewa na wewe si kwamba hampendi yule bwana, anampenda na bado anamfikiria.

Isipokuwa amefikia uamzi huo kwasababu huenda yule bwana amempuuza nk, kukubali kuolewa na wewe imetokea kama dharura tu, chaguo lake ni yule mwingine. Hivyo kwa namna moja ama nyingine yule bwana atakuja kukuvurugia ndoa yako kwa kigezo cha mtoto wake na jambo hili limekuja kuleta shida kweli.
 
Wewe umeongelea wanawake wasiojitambua ambao ni wachache mno, kuna wanawake wana watoto wameolewa na hawataaki hata kuona sura za hao walozaa nao, na wengine huenda mbali kabsaa kuwaambia watoto baba yako amekufa n.k., kwahiyo hicho unachoongea kinatokea kwa wale wasiojitambua.
 
Wewe umeongelea wanawake wasiojitambua ambao ni wachache mno, kuna wanawake wana watoto wameolewa na hawataaki hata kuona sura za hao walozaa nao, na wengine huenda mbali kabsaa kuwaambia watoto baba yako amekufa n.k., kwahiyo hicho unachoongea kinatokea kwa wale wasiojitambua.
Huwezi kusoma moyo wa mtu, ndo sababu mi nafikiri hatupaswi kufanya hivo
 
mwanamke aliyezaa anaweza kuwa yule mmewe alifariki(mjane) au yule aliye achwa kwa talaka.

wapo wanawake waliozaa kabla ya ndoa na bado hawajaolewa.

hao wote wanaweza kuolewa..
 
Na mwanaume mwenye mtoto vipi na yeye asioe?

Si bora uoe mwanamke mwenye mtoto ambaye hatakusumbua ,utaishi naye kwa furaha,amani,upendo na kuvumiliana kuliko asiye na mtoto ambaye atakusumbua,mtagombana kila siku.
Hakuna mwanaume anaeweza kuwa na furaha wakati wowote ule ikiwa mke wake anawasilina na mwanaume fulani na ambae ni mzazi mwenzake.
 
Hisia zinaweza kuwazuia watu wasifikiri vizuri, ndiyo sababu mi nafikiri tunapaswa kuwa makini sana hasa tunapofanya maamuzi kama haya.
 
Hiyo ni kwa wasiojitambua tu. Sio kila mwanamke mwenye mtoto aliachwa wengine waliachia wenyewe baada ya kujua walikosea. Pia kwa hoja yako basi hata wadada wawe makini kuolewa na wanaume waliozaa kabla ya ndoa maana huwa wanaendelea na mahusiano na wazazi wenzao au waolewe wakijua wana-share na wenzao.
 
Mkuu... Mleta mada.. Vipi umeshawahi kuwa na mwanamke mwenye mtoto ambaye sio wako!??

Maisha ya ndoa hayana fomula bhana, so husiishi kwa kuringanisha na maisha ya mwingine.

Kadhalika wapo watu wengi tuu wanaishi na wameoa wanawake wenye watoto tayari, na ndoa zao zina amani na furaha tele kabisa.

Kama wewe huwezi fanya hivyo sawa, ila usiwatishe na wengine bhana..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom