Mwanaume fanya haya

myama sana

Member
Jul 15, 2019
17
12
1. Hauwezi kumpenda mtu ambae yeye mwenyewe hajipendi.

2. Mtafute MUNGU kisha tafuta mwanamke bora. Ukiwa na hayo mambo mawili, suala la hali ngumu ya uchumi binafsi (financial freedom) litaji-solve lenyewe.

3. Mwanaume bora hapimwi kwa idadi ya wanawake aliolala nae kwa sababu 'sex' ni jambo 'cheap'. Mwanaume anapimwa kwa idadi ya wanawake aliowavua ujinga na kuwavisha maarifa.

4. Zipo aina fulani za wanawake kwa udi na uvumba unatakiwa usiwakaribie na uwakimbie kabisa. Wale wanawake wanaozani uzuri wao ndio karata ya kumpata mwanaume yeyote.

5. Sio lazima uwe kwenye mahusiano ndio uone umejikamilisha. "Relationship does not validate your existence." Unaweza ukawa single na ukaishi kwa furaha tu huku ukisubiri mtu sahihi na ofcourse atakuja tu.

6. Jifunze tabia ya kuondoka kwa yule mtu unaemhitaji sana endapo utaona hana muelekeo katika maisha yako. Kwa kufanya hivyo kunakutofautisha kati ya Mvulana na mwanaume ama Msichana na Mwanamke.

7. Usimpe MIMBA mwanamke ambae bado hujampa Mimba ya mawazo yenye tija akazaa maarifa yenye kuleta matumaini ya kuwa Mama bora.

8. Usimwite mwanamke yupo 'cheap' kwa sababu amejirahisisha mno kwako, huwezi jua. Mwanamke huyo huyo ni Mgumu kwa wanaume wengine sababu amekupenda wewe tu.

10. Wanawake na wanaume walio 'perfect' huwezi kuwapata mahala popote pale ila, wanaume na wanawake bora wako kila mahala.

11. Kama unampenda mtu mueleze wazi. Na kama upendo umeshaisha muweke wazi pia. Ni vema akaumia kwa kuambiwa ukweli kuliko kuishi kwa kudanganywa kwa matumaini hewa.

12. Ofcourse, Mwanamke ama mwanaume anaweza akakusaliti lakini MUNGU hawezi kukusaliti. Hivyo, kabla hujatafuta Partner hakikisha unae MUNGU.

Nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba,

“ No matter how strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries”

Kwa tafsiri yangu ya kuunga Wanamaanisha kwamba "haija

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom