Mwanaume bahili kwenye ndoa

Mwanaume bahili kwenye ndoa

UTASHI

Senior Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
135
Reaction score
56
Nilipata kusikia mazungumzo ya wanawake fulani,tena ni wasomi na wenye fedha zao,baadhi wakisema kua mwanaume bahili ni mzuri kua Mume kwa sababu hana tabia ya kuhonga honga wanawake/vimada na kiujumla hana wanawake wengi au hana kabisa,kwa vile wanawake wengi wanapenda hela nae hayuko tayari kutoa hela (pesa za familia zinatunzwa vizuri) na anaepuka magonjwa ya kuambukizwa (magonjwa ya zinaa),Na wengine wakisema hatoitunza familia vizuri,yaani atakua anabana kutoa hela kwa mambo muhimu ya kuendeleza familia.Hivi ndugu wana JF hii suala likoje,hivi hili suala la ubahili ni sehemu ya kuelezea ubaya au ubora wa MUME?
 
Ni vema tungepata maana ya msamiati wa ubahili ili tuweze kuchangia vizuri.kwasababu kuna watu wakipanga mambo yao hawataki yakwame hivyo kama alipanga kununua kitu fulani ni ngumu kupangalua.
 
hao wanawake awajui kwamba mwanaume anaweza kuwa mbahili ndani ya nyumba ila kwa vimada asiwe mbahili. tumeshuhudia familia zikipata shida wakat uyo baba anaonga nyumba na gari
 
Ni vema tungepata maana ya msamiati wa ubahili ili tuweze kuchangia vizuri.kwasababu kuna watu wakipanga mambo yao hawataki yakwame hivyo kama alipanga kununua kitu fulani ni ngumu kupangalua.

mtu mbahili ni mtu ambaye ni mgumu kutumia pesa au mali aliyonayo kwa wakat mnaotaka nyie atumie. kuna ubahili wa kawaida kama ambao mnauona kwa hakina mangi na ubahili uliopitiliza.
wanaume wengi ni wabahili kwa watu wa familia ila kwa wasichana anaowapenda asiwe mbahili.
 
aiseee...kikombe hiki kiniepuke
 
Kuna watu ni bahili lakini wanawake kibaooo...me nnao mfano hai..swali ni je anawapataje/wanampendea nini wakt ht chupi ya buku hajawai kuwanunulia....
 
bahili akafilie mbali huko,mwanaume bahili hashindwi kuhesabu chunguni vipande vya nyama akhuuuuu aishie huko huko.
 
1001013_541526635884070_462274060_n.jpg
 
Wanaume ni bahili kwa mkewe lakini sio kwa vimada tena unaweza kushangaa mwenzio mpaka kanunuliwa gari we unatembelea dalala.......wanaume ni headache tupu Mungu atunusuru na hili janga.



DON'T HUNT WHAT YOU CAN NOT KILL.
 
bahili akafilie mbali huko,mwanaume bahili hashindwi kuhesabu chunguni vipande vya nyama akhuuuuu aishie huko huko.

Na kipande cha samaki pia..mixa hela anahesabia mfukoni ukiomba hela unapewa ile ile kamili haina change yani hahahahaha
 
Back
Top Bottom