Mwanasheria wa serikali kukimbia tena kesi kesho ?

Mwanasheria wa serikali kukimbia tena kesi kesho ?

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Arusha,

Kesi ya kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi iliyofunguliwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kasulu ,Dahn Makanga dhidi ya Mathew Mollel inatarajiwa kuendelea kesho kwa upande wa mlamkikiwa Methow Mollel kutoa utetezi wake mbele ya hakimua anayesikiliza kesi hiyo.

Awali kesi hiyo ilishindwa kuendelea mahakani hapo kutokana na mwendesha mashtaka wa serikali katika kesi hiyo,Mary Lucas kupata dharula na kesi iyo kuarishwa hadi keshe tarehe 18 mwezi wa nane mwaka huu

Hatahivyo kesi iyo yenye mvuto kwa wakazi wengi wa jiji la arusha shaidi uyo anatarajiwa kushuhudiwa na idadi kubwa ya wasikilizaji kutokana na mvuto wa kesi hiyo.

Awali upande wa mashtaka uliwasilisha jumla ya mashahidi kumi akiwemo mkuu wa wilaya wa zamani Makanga,ofisa upelelezi kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai,Sajenti George Francis pamoja na maofisa ardhi wa jiji la Arusha walifika mbele ya mahakama hiyo kutoa ushahidi wao katika kesi hiyo inayovuta hisia za wakazi wengi wa mkoa wa Arusha.

Katika kesi hiyo nambari 430 ya mwaka 2016 Makanga ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Bariadi Mashariki alifika mbele ya kituo kikuu cha polisi cha kati na kumtuhumu mme mwenzake Mollel kughushi mukhtasari wa serikali ya mtaa wa Levolosi na kujipatia hatimiliki ya kiwanja namba 231 kitalu DD kilichopo Mianzini jijini hapa.


Mwisho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom