Mwanasheria Mkuu wa Serikali apigwe "stop" kuingia Bungeni

Mwanasheria Mkuu wa Serikali apigwe "stop" kuingia Bungeni

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,198
Reaction score
162,731
Kwa mujibu wa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,Mwanasheria Mkuu wa Serikali si mshauri wa Bunge bali ni mshauri wa serikali na kwamba Bunge lina mshauri wake wa maswala hayo ya kisheria.

Kauli hiyo mh.Lissu aliitoa bungeni na hata Mwanasheri Mkuu mwenye hakuwahi kuipinga kauli hii kwa namna yoyote ile jambo linalothibitisha kuwa mh.Lissu alikuwa sahihi kabisa.

Lakini je,kiuhalisia,mwanasheria huyu awapo bungeni,ni kweli hutoa ushauri kwa serikali tu na si kwa bunge zima?Na je si kweli kuwa huyu mwanasheria hupewa nafasi ya kuongea ndani ya bunge pengine kuliko hata wabunge wenyewe?

Alafu mwanasheria huyu anaposimama bungeni na kuchangia huwa ana tofauti gani na wabunge zaidi ya kutumia nafasi yake vibaya kutaka kuwaburuza wabunge na kuibeba serikali?

Kama kigezo ni kuwa mwanasheria mkuu wa serikali na timu yake ndio huandaa miswaada hiyo kabla ya kuileta bungeni na hivyo anapaswa kuwepo Bungeni ili kutoa ufafanuzi pale itapohitajika,mbona basi dhamira au nia njema kama hiyo haikutumika kwa aliekuwa mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Katiba na wajumbe wake kwa kuruhusiwa kuingia katika Bunge Maalumu la Katiba?

Mh.Lissu alisema Bunge lina mshauri wake wa mambo ya kisheria,kama ni hivyo,ni kwanini mwanasheria huyu wa Bunge nae asiruhusiwe kuingia ndani ya Bunge ili nae aweze kuwashauri wabunge wawapo bungeni.

Mimi si mwanasheria,lakini najiuliza kama mwanasheria/mshauri wa bunge wa mambo ya kisheria haingii bungeni,kwanini basi na huyu mwanasheria mkuu wa serikali nae asipigwe "stop" kuingia bungeni na abaki kuishauri serikali nje ya bunge tu?

Je,huu utaratibu huu wa mwanasheria mkuu wa serikali kuingia Bungeni uko duniani kote?Kama kuna nchi hazina utaratibu huu,naamini hata sisi hatuna budi kuiga utaratibu huu kwani huyu mwanasheria wetu anaonekana kutumika kisiasa zaidi awapo ndani ya Bunge.
 
Namuunga mkono tundu lisu.

Mwanasheria wa serikali anaenda pale kama nani? mshauri wa serikali ya ccm au mshauri wa hadi vyama vya upinzani? mbona historia inaonyesha wakisimama pale huwa wanatetea mambo ya ccm tu hawako balanced kwasababu serikali ya ccm ndiyo iliyowateua wataisaliti?

Vilevile, huyo akiwa bungeni ofisi yake inadoda, yeye mwenyewe apate mshahara kama AG, na marupurupu yoote ya AG, halafu apate mshahara na marupurupu kama mbunge, hivi mnajua huyo ni sawa na mbunge wa kuteuliwa, vikao vyote vya bunge anakula posho (wakati ofisini pia posho kama kawaida) huyo huwa anakula posho kuliko wabunge wote kwani yeye ni sehem mbili zote anachukua. shangingi la u AG analipata (gari moja 250mil) na shangingi la ubunge anapata.

Kila baada ya miaka mitano marupurupu yote ya ubunge anayapata, yaani huyo ni mbunge anakula vyote vya bungeni anavyopata tundu lisu halafu huku ofisini kwake pia anakula vya uAG vyoote na marupurupu yaote. ukiwa AG unatajirika ndani ya miaka mitano ushakuwa bilionea. ni dili hilo wakati akiwa pale bungeni sisi sote tumeona anatetea tu maslahi ya chama tawala wakati anabwiya kodi zetu wote.
 
Hilo nalo ni neno.

Ameingia bungeni kupata darasa kwa mwalimu wake Lisu. Anapoulizwa swali na Lisu huwa anaingiwa na kigugumizi cha utu uzima, kiatu cha Tiundu Lisu huwa kikubwa mno kukivaa. Angenusurika kama angekaa nje apewe majibu na wasaidizi wake ambao labda wanaelewa zaidi kumjibu Tundu Lisu kuliko yeye. Kile ni cheo tu na sio lazima ajue kila kitu.

Anatakiwa kuchanganya karata zake vema na hata wakati mwingine kuomba ushauri wa kina Zitto na Marando kama anataka kuitetea vizuri serikali yake. Experience haikai kwenye umri wa mtu bali hutokana na mapito uliyowahi kupambana nayo na ukachomoka kidedea. Ukweli ndio huo. Nchi inayumbayumba na kuwayawaya kwa sababu tu serikali mbumbumbu inashauriwa na wanasheria mbumbumbu. Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie.

Zile bla bla za ZIDUMU FIKRA ZA JAMAA MMOJA TU imepitwa na wakati. HAta muasisi wa mbwembwe hizo alishituka na ndio maana akaridhia kuwapo kwa vyama vingi ili kupata changamoto ya kufikiri ili nchi ipate kuendelea.
 
sasa bungeni anaenda kufanya nini? basi anapoenda bungeni asiwe na hadhi ya mbunge, vyeo viwili kwani hakuna watu wengine? halafu, ni aibu mwanasheria anayetegemewa awe neutral kufika pale halafu analalia ccm kwa kila kitu, manake chadema na cuf huyo sio wao kwasababu hayupo katikati, yupo ccm.na atasapoti chochote ccm wanachokitaka kwasababu serikali ya ccm ndio iliyomchagua. mwanasheria wa maana ni yule wa zanzibar aliyefukizwa ambaye hakutaka kuburuzwa na ccm.
 
umeshasema mwanasheria wa serikali ndani ya bunge kuna serikali na bunge ni serikali mbunge anaweza kushauliwa na mwanashiria wa mbunge
 
umeshasema mwanasheria wa serikali ndani ya bunge kuna serikali na bunge ni serikali mbunge anaweza kushauliwa na mwanashiria wa mbunge

Mwanasheria mkuu yule anatumika vivyo sivyo na serikali na ndio maana hata Lissu alimkana hadharani huku akimnyooshea kidole.

Kwa kifupi,kuna tatizo linalohitaji kuwa addressed kwa faida ya nchi.

Tuache siasa katika mambo ya msingi.
 
Hv na ule wakat wa kusema ndioooooooooooo nae uwa anakuepo???
 
Kwa upande wangu naona hapa kuna tatizo kubwa la uelewa...Dunian pote AG ni member wa Bunge, sababu. Bunge kazi yake ni kutunga Sheria na izingatiwe kuwa sheria zote zinaandikwa(drafted) na Ofisi. Ya AG sasa itakuwa haina maana kama AG haji bungeni
Lakn pia wabunge wetu Lissu inclusive wanajua kuwa nao pia wanaweza kuaandaa sheria zao bila kupitia ofisi ya AG (member's private bill) na wakaleta bungeni lakini tofauti na hapo waache wanaoandika sheria wafikie malengo. Yao

Lakini Pia Lissu pamoja na umahiri wake wa sheria anapaswa kupunguza UANAHARAKATI AWAPO BUNGENI IF HE IS TO MAKE SENSE.

I WILL ADD when the AG uses the words "Naomba kushauri" anakuwa anatumia nafasi yake kama mbunge yeyote kuwashauri wenzake wafanye maamuzi kuunga mkono his line of argument...NA IZINGATIWE Kuwa ushauri sio binding...sasa huwa sielewi LISSU huwa anapanic nini
Kwasababu yeye mwenyewe anaposimama huwa kimsingi anashauri
Na LISSU anaelewa kuwa kila mtu anatafsiri sheria husika kulingana. na jinsi alivoilewa yeye mwenyewe na ndio sababu utakuwa kesi ina mawakili pande mbili NA PIA utakuta kesi moja wamekaa majaji WATATU same ISSUES na kila jaji anatoa tafsiri yake...

LETS LEARN TO UNDERSTAND EVEN THOSE WITH DIFFERENT OPINIONS FROM.OURS
 
Mm sidhan huyo mwanasheria wa serikal kama anajua sheria vzr ndo hii ya kuteua teua kindugu, ukiwa makin sn ukiangalia bunge hil utagundugua mwanasheria ni dhaifu sn kwann nasema hv nasema hv maswal meng anayoyajibu kutoka kwa wapinzan ya kisheria hajibu kisheria, tuendelee na utaratibu huu wa buge kama lilivyozoea analeta mazoea yale yale badala ajibu hoja za wapinzan kisheria kama alivyoulizwa mambo ya kisheria pala hakuna kitu.
 
Siku za hivi karibuni mwanasheria wa serikali amekuwa akitoa ushauri au kushinikiza mambo ambayo yanaminya uhuru wa bunge. Tuambiwe majukumu yake
 
Ndio maana tunahitaji katiba bora, na si hii 'pandikizwa' ya MiCCM.
Inayotumika sasa ni katiba ya chama kimoja.
 
Mwanasheria mkuu ni Mbunge, that clarify everything
 
Huyu Mwanasheria mkuu wa sasa kiboko yaani sio kilaza ni juha kama Abu Jahli wa kwenye kitabu cha akina faizafoxy.
 
Kuna watu wanaongea pumba humu. Hasa hao wanaotumia kiingereza. Mfano Jana wabunge wakiwa kwenye semina alinyanyuka kwa hasira na kuongea pumba. Mpaka ilibidi Mbatia asimame na kumuonya kuacha kuongea vitisho kwa wabunge. Huyu mwanasheria ni kihio. Na ole wake Jana km Tundu lisu angekuwepo asingeongea ule ujinga.
 
Back
Top Bottom