Mwanasheria mkuu US atakiwa kujiuzulu kwa kuwasiliana na Urusi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mwanasheria mkuu nchini Marekani jenerali Jeff Sessions alikutana na balozi wa Urusi wakati wa uchaguzi licha ya kuthibitisha kuwa hakufanya mawasiliano yoyote na Urusi.

Idara ya haki ilithibitisha kuwa alikutana na Sergei Kislyak mnamo mwezi Julai na Septemba mwaka uliopita ikiwa ni miongoni mwa majukumu yake katika kamati ya bunge la seneti ya huduma za usalama.

Bw Session alisema kuwa matamshi yake yalifananishwa na jukumu lake katika kampeni ya rais Trump.

Madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani yamemkabili rais Trump.

Idara ya ujasusi inaamini kwamba udukuzi unaodaiwa kufanywa na Urusi dhidi ya mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton ulifanywa ukiwa na lengo la kumsaidia bw Trump kumshinda Clinton.

Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Trump Michael Flynn alifutwa kazi mwezi uliopita baada ya kuidanganya ikulu kuhusu matamshi yake na bw Kislyak, kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi

Chanzo: BBC
 
Trump anatakiwa awe na serikali mpya..!


Us officials walikuwa corrupted sana! Otherwise ataisoma number
 
Wafuasi wa Clinton wanasumbuliwa na wivu tu. Trump ataishiwa miaka yake bila kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Aangalie amekaliwa vibaya na mahasimu wake
 
Back
Top Bottom