Mwanasheria Mkuu kuunganishwa rufaa ya Lema

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Ijumaa, Septemba 21, 2012 06:11 Na Eliya Mbonea, Arusha

Kurasa 1 kati ya 3
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande, amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuunganishwa katika shauri la kupinga hukumu ya kuvuliwa ubunge wa Godbless Lema (CHADEMA) kama mtu muhimu.

Akiongoza Jopo la Majaji wanaosikiliza Rufani ya Lema ambao ni Jaji Natalia Kimaro na Jaji Salum Massati, Jaji Mkuu alitoa amri fupi ya kutaka Mwanasheria aunganishwe kutokana na umuhimu wake katika shauri hilo.

“Kwa kuzingatia kanuni ya 4 (2) a, ya Kanuni za Mahakama za Rufaa 2009, na baada ya kusikiliza pande mbili za Mawakili juu ya uwezo wa kisheria wa Mwanasheria Mkuu, ambaye katika kesi hii alikua mjibu madai wa pili, zipo sababu za msingi za kuunganishwa kama mtu muhimu,” alisema Jaji Mkuu Chande.

Awali kabla ya kutolewa amri hiyo fupi ya kutaka Mwanasheria Mkuu kuunganishwa katika rufani hiyo, kulitokea mvutano wa kisheria baina ya mawakili wa pande zote mbili, juu ya ushiriki wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake, Wakili Mwandamizi, Method Kimomogoro, anayemwakilisha Lema, aliliomba Jopo hilo kuamuru Mwanasheria Mkuu aunganishwe katika kesi hiyo kama rafiki wa Mahakama na kuhakikisha haki inatendeka kwa kutoa ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kisheria.

Katika hatua hiyo, Wakili Modest Akida, anayewawakilisha wajibu rufani alikubaliana na ombi hilo, hata hivyo, Wakili wa Mwanasheria wa Serikali, Timon Vitalis, kwa upande aliliambia jopo hilo kuwa hakuwa na pingamizi.

“Hatuna pingamizi juu ya mwanasheria mkuu kuwa sehemu ya rufani hii. Lakini hatutambui anatakiwa kuwa upande gani wa mrufani au mrufaniwa kwa kuwa wakati wa kesi alikuwa mdaiwa wa pili,” alidai Vitalis.

Pamoja na mambo mengine, katika majadiliano hayo ya kisheria na uamuzi uliotolewa na Jopo la Majaji, mawakili wa pande zote walikubaliana na amri hiyo.
 
Back
Top Bottom