Mwanasheria Mkuu amuasa DPP

Mwanasheria Mkuu amuasa DPP

wanajuana hawa, wote wako kwenye system, hii ni danganya toto siku ziende.
 
Kuna faida gani kumshtaki mtu mahakamani kwenye kesi ya jinai na kumpotezea muda wake zaidi ya miaka 3, huku ukijua kwamba huwezi kumtia hatiani kwa kuwa tayari uliwapata na kuwaachia watuhumiwa halisi?

Jibu lako liwekwe kwenye katiba ya nchi kwamba "serikali iweze kushitakiwa kwa kumpotezea raia muda wake wa maisha na adhabu yake ni kumlipa fidia kwa gharama, muda na kiwango cha msongo wa maisha waliyompotezea mtuhumiwa" Miaka mitatu bila hatia imtoe mtu umaskini.
 
nilishawahi kufany akazi wakili wa serikali kabla sijajitegemea ndugu. huyo dpp nilishafanya naye kazi. kusema ukweli, hakuna jamaa anayechukia rushwa kama huyo. tatizo linalokuja hata kufanya kesi ziondolewe ni kwamba, POLISI HUWA HAWAPELELEZI KESI VIZURI, hivyo mwendesha mashitaka anafikia kipindi anaona haiwezekani kuendelea kwasababu hatutashinda kesi, na kesi ikishatoka hukumu akawa convicted that means hawezi kufungua upya kwa mambo yaleyale, option inakuwa ni kufuta kesi na kukamata tena, au kufuta kesi na kuagiza polisi wafanyie uchunguzi kitu fulani unachoona kina matatizo, upelelezi wakishakamilisha tu unakamata yule mtu na kuanzisha tena. ukisubiri hadi hukumu, basi, hukumu ikitoka huwezi kuanza upya charge ile na inakuwa ngumu kukata rufaa kwa ushahidi uliopo.

nilishawahi kuendesha kesi nyingi sana hapo kisutu, amini usiamini, polisi hao unao waona wananunua sana kesi, wanaiba na kunyofoa sana statement kwenye jalada na ndio ambao huwa wanaharibu kesi.

TATIZO LILILOPO NI KWAMBA, dpp huwa hawaelewani na Werema pamoja na masaju (dag) ambao hawa wote ni maboss wake dpp. pale ofisi ya mwanasheria mkuu kuna ukanda sana, wanapendeleana kikanda. go ask anyone who works there now, ndio maana watu tulikimbia hii ofisi, WATU WA UKANDA WA KANDA YA ZIWA ....nikimaanisha wakurya,wajaluo, yaani watu wote wa musoma na ukerewe ndio wanaokula bata ofisi hii. na ndio wanaoandaliwa na kupandishwa vyeo na kuandaliwa kuchukua ofisi baada ya maboss hao kuretire 2015 kama masaju ataendelea.

kuna vita kubwa sana kati ya hawa watu kiasi kwamba mtu kama ni mchagga yaani mtu wa kanda ya kaskazini lets say labda mchagga mtu wa arusha, tanga etc, huna chako pale na safari unanyimwa. ukiwa mtu wa kanda ya kusini kidogo wanaona aibu, lakini ukienda ofisi yao kule AGC kivukoni front, wamejaa watu wa musoma na ukerewe na ukiwa hivyo ndio wanaopandishwa vyeo na kuandaliwa kuendeleza tabaka wakubwa hawa wakiondoka.

huwezi amini DAG masaju huwa anachukia kwasababu wanaona dpp anafanya kazi bora kuliko wao na anatambulika kuliko wao. dpp anachukiwa hata kuwa na bodigadi tu wakati mwajiri wake masaju hana bodigadi, wasukuma wanapata shida (dpp ni sukuma) kwasababu tu ya dpp kuchukiwa na mwajiri ambaye ni masaju ambaye zamani alikuwa junior wake yaani dpp kwa cheo ni principal state attorney na masaju hakufikia cheo hicho. dpp aliteuliwa kutokea ofisi ya incharge mwanza kwasababu ya uchapakazi na hakika yake hakuna mchapa kazi kama huyu jamaa.

dpp amefungua ofisi za mwanasheria mkuu mahali kwingi ili huduma isogee karibu na wananchi, masaju na werema wanamchukia kwasababu wnaaona akifanya hivyo anaongeza wafanyakazi na fungu litagawanywa kwa watu wengi na kuwa halitoshi kwao kupata edp. kumbuka kuwa ni muhimu sana ofisi ya mwanasheria mkuu kuwa karibu hadi wilayani (jambo ambalo dpp amefanya) ili kesi mfano za mauaji jalada lisisafirishwe hadi mikoa mingine kwa opinion tu mfano; monduli imefunguliwa ofisi hivyo hawatakuwa wanadepend na arusha tena.

TATIZO SIO DPP KATIKA YOTE HAYA, TATIZO NI WEREMA NA MASAJU kwa ukabila na ukanda wao. kama hauamini maneno yangu, utaona nani atakuwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2015, ametoka ukanda gani, ndipo utaikumbuka hii meseji. nimeongea kwa uwazi, kwasababu niliichukia hii ofisi hadi nikaondoka kwasababu mimi sitoki ukanda huo wa werema na masaju, nikanyanyapaliwa hata kuacha kazi. watu wabaya sana hao. kama hauamini uliza wakili yeyote wa serikali ambaye sio mkurya au mjaluo, atakupa ukweli wote.

Acha ukabila wewe,kwani wewe na DPP mnatoka mkoa gani?hamtoki mkoa mmoja nyie?acheni hizo.
 
Back
Top Bottom