nilishawahi kufany akazi wakili wa serikali kabla sijajitegemea ndugu. huyo dpp nilishafanya naye kazi. kusema ukweli, hakuna jamaa anayechukia rushwa kama huyo. tatizo linalokuja hata kufanya kesi ziondolewe ni kwamba, POLISI HUWA HAWAPELELEZI KESI VIZURI, hivyo mwendesha mashitaka anafikia kipindi anaona haiwezekani kuendelea kwasababu hatutashinda kesi, na kesi ikishatoka hukumu akawa convicted that means hawezi kufungua upya kwa mambo yaleyale, option inakuwa ni kufuta kesi na kukamata tena, au kufuta kesi na kuagiza polisi wafanyie uchunguzi kitu fulani unachoona kina matatizo, upelelezi wakishakamilisha tu unakamata yule mtu na kuanzisha tena. ukisubiri hadi hukumu, basi, hukumu ikitoka huwezi kuanza upya charge ile na inakuwa ngumu kukata rufaa kwa ushahidi uliopo.Tunashukuru kwa kutu "ALART" kuwa huyu DPP "sometimes" anaondoa kesi mahakamani kwa sababu ya kupewa rushwa...
Aliwahi kuandika Mwandishi Kondo Tutindaga na Joster Mwangulumbi kwamba serikali ya Rushwa hakuna lisilowezekana sasa unashangaa werema kuwa mkabila?Mbona masaju na werema ni vinara wa ukabila sana wakiongozwa na JK anayewavumilia....Hakuna jambo zuri kwenye utawala huu wa wala rushwa na wasiojua nini maana na Urais,AG nk...Dini kabila rangi fedha na uchi ni nguzo za Ccm kuongoza nchi kutoka Ikulu mpaka kijijinikumbeeeeeeeeeeeeee!ukabilaaaaaaaaa!!!!!
tatizo linalokuja hata kufanya kesi ziondolewe ni kwamba, POLISI HUWA HAWAPELELEZI KESI VIZURI,
Walau jana he talked senses! Nasikia huwa yuko humu mitandaoni, akifuatilia fuatilia maoni ya wadau! Alozungumzia juu ya haki for peace not the other way round, mmh!
Kwako Werema: Je kesi inapofutwa kwa sababu za kiufundi ndio haiwezi kurekebishwa na kurudishwa shitaka? Kuna tukio la hivi karibuni ambapo shirika moja la umma limeuzwa kwa bei ya kutupa na fedha yake kuingizwa mfukoni kwa wakuu wa shirika. Sasa kesi imefutwa na DPP, ndio kusema shirika na fedha ya umma imeondoka?Mwanasheria Mkuu amuasa DPP
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Jaji mstaafu Frederick Werema ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kuacha kuondoa mashitaka mahakamani bila kuwasiliana na wapelelezi, ili kuondoa vitendo vya rushwa. Alisema hayo jana mjini hapa katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa, wakati akifungua mkutano wa mawakili wa Serikali wafawidhi, wakuu wa upelelezi wa makosa ya jinai na vikosi vingine vya Polisi.
Jaji Werema alitaka uondoaji wa mashitaka mahakamani, uwekewe utaratibu wa ndani, ili wapelelezi wataarifiwe ni kwa sababu gani kesi inaondolewa kupitia tamko la DPP la kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi, kwa kuwa uamuzi kama huo unahitaji uwazi, ili kuondoa hofu ya rushwa na dharau kwa upande mwingine.
Mwanasheria huyo wa Serikali alisema nchi sasa inahitaji msaada wa Mungu kuliko wakati wowote, kutokana na kuongezeka kwa uhalifu na tabia ya watu kutotii sheria. Alitaka wapelelezi na waendesha mashitaka, kuwa na ushirikiano wa karibu na kusisitiza kuwa ushirikiano huo ni lazima na si hiari.
Jambo hilo ni lazima si hiari, hakuna kati yenu anayeweza kufanikisha haki katika jinai, bila kwanza kusaidiwa na mwingine. Mpelelezi anahitaji kuthaminiwa, kuelezwa anachotakiwa kuongeza katika upelelezi, ili kosa lithibitike pasipo shaka, alisema Jaji Werema.
Alitaka mawakili wa Serikali, kuacha kutunishiana misuli na wapelelezi na hata kwa mahakimu na majaji huku akikemea tabia ya kudharauliana kutokana na elimu.
Pamoja na DPP kutoa makusudio ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi, Jaji Werema alisema wapo wapelelezi wamekuwa wakifanya kazi kwa ufanisi kutokana na uzoefu wa kazi waliokuwa nao. Nguvu kwa wahalifu Alitaka yatumike maadili wakati wa kukamata wahalifu, kwani hata sheria inaruhusu matumizi ya nguvu kwa kufuata utaratibu.
Alisema hata kwenye mikusanyiko ya watu, Sheria inasema hadhari itolewe mara tatu, lakini kinachoonekana nguvu zaidi zimekuwa zikitumika ikiwemo matumizi ya mabomu ya kutoa machozi na hata kupiga wananchi risasi.
Usimpige mtu risasi kichwani au mgongoni, hilo ni kosa, kwa sababu mmejifunza hiyo kazi, kwa nini usimpige mguuni?
Alihoji Werema na kuitaka polisi kuacha kutumia silaha ovyo katika kudhibiti uhalifu. Wizi benki Pia alitaka ufanyike utafiti na mapendekezo ya kutunga sheria au kuongeza adhabu, kwa watu wanaoiba fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM), katika benki kwani wizi huo umekuwa ukiharibu uchumi wa nchi.
Tatizo ni sheria, adhabu inayotolewa ni ndogo. Ukienda Uganda adhabu yake ni miaka 25, ndiyo maana wahalifu wengi wa benki wamekuwa wakikimbilia Tanzania kutokana na adhabu kuwa ndogo, alisema.
Source: HabariLeo
nilishawahi kufany akazi wakili wa serikali kabla sijajitegemea ndugu. huyo dpp nilishafanya naye kazi. kusema ukweli, hakuna jamaa anayechukia rushwa kama huyo. tatizo linalokuja hata kufanya kesi ziondolewe ni kwamba, POLISI HUWA HAWAPELELEZI KESI VIZURI, hivyo mwendesha mashitaka anafikia kipindi anaona haiwezekani kuendelea kwasababu hatutashinda kesi, na kesi ikishatoka hukumu akawa convicted that means hawezi kufungua upya kwa mambo yaleyale, option inakuwa ni kufuta kesi na kukamata tena, au kufuta kesi na kuagiza polisi wafanyie uchunguzi kitu fulani unachoona kina matatizo, upelelezi wakishakamilisha tu unakamata yule mtu na kuanzisha tena. ukisubiri hadi hukumu, basi, hukumu ikitoka huwezi kuanza upya charge ile na inakuwa ngumu kukata rufaa kwa ushahidi uliopo.
nilishawahi kuendesha kesi nyingi sana hapo kisutu, amini usiamini, polisi hao unao waona wananunua sana kesi, wanaiba na kunyofoa sana statement kwenye jalada na ndio ambao huwa wanaharibu kesi.
TATIZO LILILOPO NI KWAMBA, dpp huwa hawaelewani na Werema pamoja na masaju (dag) ambao hawa wote ni maboss wake dpp. pale ofisi ya mwanasheria mkuu kuna ukanda sana, wanapendeleana kikanda. go ask anyone who works there now, ndio maana watu tulikimbia hii ofisi, WATU WA UKANDA WA KANDA YA ZIWA ....nikimaanisha wakurya,wajaluo, yaani watu wote wa musoma na ukerewe ndio wanaokula bata ofisi hii. na ndio wanaoandaliwa na kupandishwa vyeo na kuandaliwa kuchukua ofisi baada ya maboss hao kuretire 2015 kama masaju ataendelea.
kuna vita kubwa sana kati ya hawa watu kiasi kwamba mtu kama ni mchagga yaani mtu wa kanda ya kaskazini lets say labda mchagga mtu wa arusha, tanga etc, huna chako pale na safari unanyimwa. ukiwa mtu wa kanda ya kusini kidogo wanaona aibu, lakini ukienda ofisi yao kule AGC kivukoni front, wamejaa watu wa musoma na ukerewe na ukiwa hivyo ndio wanaopandishwa vyeo na kuandaliwa kuendeleza tabaka wakubwa hawa wakiondoka.
huwezi amini DAG masaju huwa anachukia kwasababu wanaona dpp anafanya kazi bora kuliko wao na anatambulika kuliko wao. dpp anachukiwa hata kuwa na bodigadi tu wakati mwajiri wake masaju hana bodigadi, wasukuma wanapata shida (dpp ni sukuma) kwasababu tu ya dpp kuchukiwa na mwajiri ambaye ni masaju ambaye zamani alikuwa junior wake yaani dpp kwa cheo ni principal state attorney na masaju hakufikia cheo hicho. dpp aliteuliwa kutokea ofisi ya incharge mwanza kwasababu ya uchapakazi na hakika yake hakuna mchapa kazi kama huyu jamaa.
dpp amefungua ofisi za mwanasheria mkuu mahali kwingi ili huduma isogee karibu na wananchi, masaju na werema wanamchukia kwasababu wnaaona akifanya hivyo anaongeza wafanyakazi na fungu litagawanywa kwa watu wengi na kuwa halitoshi kwao kupata edp. kumbuka kuwa ni muhimu sana ofisi ya mwanasheria mkuu kuwa karibu hadi wilayani (jambo ambalo dpp amefanya) ili kesi mfano za mauaji jalada lisisafirishwe hadi mikoa mingine kwa opinion tu mfano; monduli imefunguliwa ofisi hivyo hawatakuwa wanadepend na arusha tena.
TATIZO SIO DPP KATIKA YOTE HAYA, TATIZO NI WEREMA NA MASAJU kwa ukabila na ukanda wao. kama hauamini maneno yangu, utaona nani atakuwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2015, ametoka ukanda gani, ndipo utaikumbuka hii meseji. nimeongea kwa uwazi, kwasababu niliichukia hii ofisi hadi nikaondoka kwasababu mimi sitoki ukanda huo wa werema na masaju, nikanyanyapaliwa hata kuacha kazi. watu wabaya sana hao. kama hauamini uliza wakili yeyote wa serikali ambaye sio mkurya au mjaluo, atakupa ukweli wote.
Kwako Werema: Je kesi inapofutwa kwa sababu za kiufundi ndio haiwezi kurekebishwa na kurudishwa shitaka? Kuna tukio la hivi karibuni ambapo shirika moja la umma limeuzwa kwa bei ya kutupa na fedha yake kuingizwa mfukoni kwa wakuu wa shirika. Sasa kesi imefutwa na DPP, ndio kusema shirika na fedha ya umma imeondoka?