nonino
Member
- Apr 11, 2012
- 32
- 12
Kuna mwanasheria mdada mmoja, anataka ktk familia nzuri tu kifedha na kielimu. Huyu mwanasheria umeenda kidogo ila akawa hajaolewa, bi huyu akaanza mahusiano na mume wa mtu, mkewe huyo baba kipindi hicho alikuwa mwaka wa pili pale mlimani akisoma sayansi ya jamii. Huyu binti mwana sayansi ya jamii sio mkubwa sana kiumri ila mumewe ni mkubwa kidogo yuko age moja na huyo mwanasheria. Mwanasheria huyu sasa baada ya kuonja asali badala ya kula kimya kimya yeye akaanza nyodo. Mara ampelekee lunch mume wa mwenzio mpaka ofisini kwake, akawa anaenda mpaka nyumbani kwa huyu baba bila aibu, mara amfate mwenye Mali chuoni kumfanyia fujo, yani kwa ufupi alikuwa anamfanyia mwenzio vurugu kibao. Watu tukawa tunashangaa huyu binti mwana sayansi ya jamii yeye yuko kimya wala alikuwa ataki vurugu kabisa, kwa kifupi watu walikuwa wanamuona mjinga.
kubwa ya yote sasa, huyu mwanasheria akaamua kubeba mimba ya huyu baba,na kuzaa wakati huo huyu baba tayari mkewe naye alikuwa na mimba ya mtoto wao wa pili baada ya kumaliza Chuo, maana alimaliza high school akiwa na ujauzito aliopewa na huyu huyu mumewe so aliolewa muda mfupi baada ya kumaliza shule.
Mume wa mtu baada ya kumjaza mimba huyu lawyer, Ndio akakumbuka ooh kuwa yeye ni mume wa mtu. Mpenzi yao sasa yakageuka vita lawyer anataka wakafunge Ndoa bomani huyu mwanaume hataki akamwambia yy ana mke wake, na hataki mtoto wa nje wala mke wa pili, kwa ufupi wakaachana kwa vurugu kubwa sana, mwanaume aka kubali kutunza mtoto.
Usichoke, sasa bwana baada ya huyu lawyer kujifungua mtoto wa kike, alipo fikisha mwaka mmoja huyu mwana sayansi ya jamii akamwambia mumewe kila week end awe anaenda mchukua huyo mtoto wake wa kike(wa nje) maana wao wan watoto wawiliwa kiume ili awazoee ndugu zake na yy baba yake tangu mapema. Baba kafata ushauri wa mkewe kamwambia ex wake naye bila kufikiri mara mbili akakubali, mtoto kila ikifika ujumaa anaenda kwa baba yake mpaka JUMAPILI jioni ndio anarudishwa kwa mama yake. Kumbe huyu mwana sayansi ja jamii ana lake moyoni, kumbe alikuwa anatafuta tu sababu ya kuwa karibu na Yule mtoto wa nje wa mumewe ili afanye yake. Huyu mama mwana sayansi ya jamii akawa anakaa vizuri tu na Yule mtoto wa mumewe, tena mtoto akawa anampenda sana tu mama ake wa kambo, hali ikawa shwari , mtoto alipofikisha miaka Sita hapo ndio kasheshe ilipoanza.
Huyu mtoto akaanza darasa la kwanza ni mtoto ambaye kichwani yuko vizuri. Mtoto akamwambia mama yake mzazi mi nataka kwenda kukaa na baba yangu moja kwa sitaki kukaa na wewe, mama akakataa mtoto akatoroka akaenda kwa baba yake. Mama yake kumfata kwa baba yake mtoto akawa anakataa kurudi kwa mama yake, mwanasheri akawa juu anadai mwanae huku mtoto nae analia hamtaki mam yake, basi mwanasheria akawpigia simu ndugu zake wakaja na polisi, wao kumbe wamewaambia wale polisi waje kumkamate Yule baba wakamuweke ndani. Polisi tena wamekuja na gari kabisa, iliwalipofika pale kuona ile hali kwamba ni mtoto ndie anayemkataa mama yake sio kwamba baba yake anamzuia asiende kwa mama yake, ikabidi waaambie wazazi na mtoto wao wote wapande kwenye gari waende kituoni, kufika polisi mtoto anauizwa unataka uende nyumbani na nani anajua baba mi mama simtaki. Yule mwanasheria unaambiawa alikuwa anafanya fujo kama chizi, basi akamwambia Mkuu wa kituo unamuona alivyo mi ndio maana sitaki kuishi naye, basi polisi wakamua mtoto aendoke na baba yake.
kesho yake mama mtu akawa anataka kwenda mahakamani , ndugu zake wakamkalisha kikao wakamwambia ww achana na mambo ya mahakamani , tatizo ni mtoto hakutaki sio baba ana mkatalia mtoto, bi dada ndio kuamua kwenda ustawi wa jamii basi mtoto sasa alipo ulizwa kwa nini hataki kukaa na mama yake, mtoto anawambia maafisa ustawi nyiyi wenyewe mnajua ili mtoto akuwe vizuri lazima Aishi na baba na mama, na mimi mama huyu simtaki anaonyesha mama yake mzazi kwanza huyu aliiba mume wa mtu, mi nikishii naye atanifundisha tabia mbaya mi nataka niishi na baba na mama huyu( anamuonysha step mother wake). Mama yake alilia, basi mtoto wakamua aendelea kukaa kwa baba yake. Basi mwanasheria wa watu akamfata mwana sayansi ya jamii nyumbani kwake etiquette anamuomba msamaha amsmehe yeye alikuwa anafikir kwamba mtoto wake mwenzie amemfanyia dawa za Kiswahili ili amkatae mama yake.
Akawa anamwambia mwana sayansi ya jamii, jamani we mwenyewe umezaa unajua mtoto anavyouma kama kuna
una kitu umefanya nisamehe Yale ya zamani yamepita. Mwana sayansi ya jamii naye akamjibu sio mtoto tu anayeuma mume naye anauma pia, we Yale yote ulionifanyia Leo unajifanya umesahau, mi sijasahau na wala sitasahau, na mimi nimefanya kumtumia mwanao ili nikuumize, mi sijamroga ili nimeyumia elimu yangu ya darasani kumfanyia awe vile ninavyotaka,
Sasa hivi mtoto yuko darasa la tatu, bado hamtaki kabisa mama yake mzazi yaani hata akimfata kwa baba yk ili a salimie mtoto anakuwa hataki, mpaka mama mzazi anamuomba mama mlezi amubembeleze mtoto ili aje amsalime, yani huyo mwanasheria unaambiawa Hana raha full mawazo. Siku hizi amekua mpole na heshima a nayo.