Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,189
- 3,548
Kumekuwa na tabia ambayo serikali imekuwa ikifanya jambo ambalo limetuathiri sisi wananchi na hakika kama hatutabadilika basi usafi hautakuja kuwa utamaduni wetu. Kuna hii desturi ya kufanya usafi wa uhakika pindi kunapokuwa na ziara za viongozi wakuu. Nadhani kwa mrundikano wa "Perfume zetu huko mitaani" serikali hutumia kiasi kikubwa sana cha fedha kuondosha "lumbesa za taka taka mitaani.
Ili kutufunza tabia njema sisi wananchi wazazi wetu walitakiwa kutuhimiza kufanya usafi mwili mzima tangu tukiwa wadogo lakini siyo hili zoezi la kutuhimiza "kunawa uso Obama anakuja" Ikiwa Obama huyu angeamua yeye binafsi kuitembelea Dar es Salaam sehemu yoyote hakika angegundua kwamba kumbe tumenawa uso pekee bali makwapa yetu yana uoto asilia.
CCM Oyeeeee!!!!