Mwanangu hataki kula

Mwanangu hataki kula

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,040
Reaction score
2,009
Habari zenu watanzania,mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.Tatizo lake hataki kula chochote tofauti na kunyonya tu.

Nilishanunua dawa za minyoo katumia mpaka basi,nikanunua vitamni B complex labda atapata hamu ya kula wapi, najitahidi kumbadilishia vyakula yofauti.

Anachokunywa ni maziwa kwani nimemuekea bili na kunyonya tu.Mm nataka angalau ale chakula lakini ndoo ukimpa ni kilio na anavitema kabisaaa hataki kabisaa.

Sasa nisaidieni mawazo ndugu zanguni make hapa JF ni uwanja mpana sana.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu watanzania,mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.Tatizo lake hataki kula chochote tofauti na kunyonya tu...

 
Habari zenu watanzania,mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.Tatizo lake hataki kula chochote tofauti na kunyonya tu ,nilishanunua...
Welcome to the parenthood. Ni upepo utapita ila kama hatapiki mlazimishe kunywa uji au maziwa ya lactogen2 angalau akimeza vijiko 8 inatosha.

NB: unamlazimisha ikiwezekana hata kwa kumkaba hakuna huruma HAFI😅😅😅
 
Unataka kumtafutia mdogo wake nini
Muwekee chakula kwenye sahani na wenzake, au kama ni uji usimnyweshe akiwa peke yake tafuta watoto wawili wa jirani uwe unawapa zamu zamu, atazoea tu kula
 
Mama yake anapikaje chakula?? Ukute michumvi na uji unamasukari mtoto haelewi!!

Mama yake alimnyonyesha kwa miezi sita kabla ya kumwanzishia chakula?? Ukute alianza kumpa kula kabla sasa mtoto amekinai

Kama vyote vimeshindikana mtoto asinyonyeshwe wala kupewa maziwa mpaka ale inaelekea anashiba hayo maziwa hiki kikishindikana

Mtoto akiwa analishwa asikabwe, yan mama asitumie nguvu kabisa awe natabasam kama ikibidi wacheze, muekee vikatuni au nyie wakati mnakula na yeye mlishe sio anakula peke yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom