Mwanangu anateseka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanangu anateseka!

Discussion in 'JF Doctor' started by Amoeba, May 2, 2011.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  My youngest son is 10 m.o,miezi miwili sasa anasumbuliwa na vipele sehem za makalio, vidogovidogo sana - kama ukurutu vile! Vinamuwasha sana, hasa wakati wa usiku-anajiuna mpaka usingizi unapompitia, na akishtuka tena analia na kujikuna. Tumeenda hospial mara kadhaa, kila tukipewa dozi akimaliza tatizo haliishi (three times, different med!!). Kuna dawa ya kupaka ambayo tulishauriwa na dr tuwe tunampaka sambamba na dawa za kumeza: dawa hizi zinamsaidia sana kuondoa vipele, lakini dozi ikiisha tusipompaka hali inarudi vilevile, im worried! Wakuu, hii inaweza kuwa nini? Wataalamu ushauri tafadhali!
  Afya yake iko poa sana tu, tatizo anapoanza kuwashwa tu: amani yake na yetu sisi wazazi inakwisha kabisaa!!!

  Heelp!
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Mkuu, wala usichelewe ichukulie serious hii kitu, nenda moja kwa moja kwa dr wa magonjwa ya watoto usimtese bure mtoto!
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .......pole sana kamuone Dr wa magonjwa ya ngozi, pale upanga jirani na muhimbili kuna clinic ya Dr matthew. Huyu Dr ni bingwa wa magonjwa ya ngozi anaweza kukusaidia.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  It could be allergy! Jaribu vipimo pale natural therapy karibu na Hindu mandal
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nafikiri ni Allergy kama alivyosema Gad....pale Muhimbili wanafanya allergy test nakushauri uende na mwanao.

  Pole sana Amoeba, atapona,Mungu na amsaidie awe mzima mapema!AMEN
   
 6. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa maoni yangu mpe dawa za minyoo naamini tatizo litaisha kama unasoma net sana search pinworms i guess ndo zinamsumbua coz mara nyingi hata kwa wa2 wazima pinworms zinasumbua usiku zaidi,tafuta dozi nzuri ya minyoo mpe,pole sana,
   
 7. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  In the mean time wakati unatafuta ufumbuzi kwa daktari wa watoto au daktari wa ngozi....acha au punguza matumizi ya pampers especially kama zinakaa muda mrefu, huwa zinasababisha 'nappy rash', au pia inaweza akawa na allergy material ya hizo pampers. Mvishe nappy za kawaida za cotton lakini uwe makini kumbadilisha haraka mara tu anapojisaidia, kisha unafua vizuri na kuanika ikauke kabisa kabla ya kumvisha tena.
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Shukrani kwenu wakuu kwa msaada wa mawazo!
  I promised to take care of him since yuko tumboni, nitatumia gharama zozote kuhakikisha anapata tiba.
  Nisaidieni contact za Dr anayeweza kunisaidia, popote pale alipo.
  Nawashukuru sana wakuu!
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Pole sana Mkuu kwa hilo tatizo. Kwa mzazi yeyote ambaye ni responsible..mtoto akiumwa lazima amani ndani itatoweka. Kama walivyosema wadau, inawezekana mtoto ana allergic reaction na baadhi ya vitu mnavyotumia au ni maambukizi. Kwa hiyo jaribu kuchukua hatua zifuatazo haraka.
  1. Acha kutumia pampers anazotumia na badala yake tumia vitambaa vya pamba au nepi. Pia badili hata sabuni anayotumia na poda kama mnaitumia kupunguza unyevunyevu.
  2. Mtafute kwanza daktari bingwa wa watoto ili amchunguze na kukupa ushauri wa kitaalamu.
  3. Wakati huo endelea kupeleleza wapi unaweza kumpata wataalamu wa magonjwa ya ngozi/allergy.
   
 10. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kwa jinsi tatizo unalozungumzia ni vizuri sana ukafata ushauri wa riwa hapo juu. vipele vidogo sehemu hizo ulizo taja usabishwa sana na kuto mbadirisha mtoto wakati muafaka anapojisaidia haja nogo au kubwa. Kitu kingine labda joto kali sana labda ujaribu kumuacha kidogo mda mwingine apate hewa au kumpangusa kwa taulo lenye maji hili kama kuna jasho linatoka na joto litamsaidia kupunguza joto.

  Kitu kingine labda yuko allergic na material inayotumika kama ni diaper au nepi. Ukimbadirisha weka poda inasaidia pia na pia ningekushauri utafute dawa inaitwa A+D original ointment kama hipo madukani inaweza kukusaidia ni nzuri sana kwa watoto wanaopata vipele kutokana sababu hizo nilizo taja.
   
 11. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kuongezea ukimbadilisha nepi msafishe kabla ya kumvalisha nepi safi. Pia kwa vile hali ya hewa ni joto kali avae nepi tu bila lichupi lenye plastik.
   
 12. U

  UNIQUE Senior Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Mie nikisikia mtoto anaumwa roho yangu inakosa amani kabisa....pole nimekosa hata maneno haki ya Mungu vile huruma iliyonishika haielezeki pole dear
   
 14. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Pole mkuu jitahidi kuwaona wataalam wa mzio mtoto apate nafuu haraka
   
 15. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  watoto wanauma sana wauguapo. pole sana. nadhani waone specialists wa ngozi na pima allergy kama waungwana walivyoshauri. Ila i symphasize na wewe kwa mwanao. every parent should.
   
 16. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Pretty na wadau wengine tafadhali nina tatizo kama hili kwa mwanangu wa kike (5 yrs old). Yeye ameanza ghafla tu kuwashwa mwili mzima. Tumejaribu hospital za huku mkoani lakini hakuna nafuu na hali inaendelea kuwa mbaya kwani vipele vinasambaa sasa mwilini. Je mnaweza nisaidia namba ya huyo Dokta au specialist yeyote anayefahamika kwa magonjwa kama hayo walao nimpigie kuomba appointment maana niko nje ya Dar tafadhali.
   
 17. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  pole sana Amoeba,

  Mimi mwanagu alinisumbua sana kwa tatizo kama lako akatibiwa hospital mbalimbali ikiwamo KCMC lakini haikusaidia zaidi vipele vikawa vinakauka na kifanya ngozi kuharibika na baadae vunarudi!!!

  Mungu alinisaidia nikagiziwa na mtu Dar kuna clinic inaitwa alt sinza walichofanya walimckua damu kama ya malaria kesho nikafata majibu wakaniambia mwanangu alkua na aleji ya irish potatoes(yaani viazi vya chips) walinanzishia dawa akapona vizuri kabisa......... na bei zao si kubwa ukilinganisha na nilivyokwishahangaika!

  Mtoto akiumwa hata nyumba inakua haina raha wala amani!
   
 18. L

  Leornado JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pia joto linachangia sana watoto kuwashwa sehemu za siri, fata ushauri wa kumbadilisha nepi mara kwa mara na hakikisha anapata hewa ya kutosha huko chini ili kuzuia jasho linalomsababishia rushes na kuwashwa. Hali ikizidi kuwa mbaya muwahishe hospitalini.
   
 19. m

  mkisah2 Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama sio allergy basi itakuwa SCABIES...

  kama muonekano wa vipele upo kama kwenye hizo atachments basi nunua scaboma lotion mwogeshe na umpake alale nayo kwa usiku mbili..usimpe BBA 25% kama ni chini ya miaka miwili ila wote mjipake BBA kwa 24h kwa siku mbil(itreat all the house hold)..fua ngo zenu kwa maji moto
  ila its better kama utampeleka kwa wataalamu ama piga picha vipele na u upload humu kwenye JF

  imagesCAZL33UO.jpg imagesCAOHTSRA.jpg imagesCA2VSMBP.jpg
   
 20. m

  mkisah2 Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sehemu za matajo mikunjo ja mikono na miguu na kichwa ni maeneo yanayoathrika zaidi....na picha hapo juu zinaonesha muonekano wa vipele kama mtoto ni mwepe ama kama ni mweusi...kwa maelezo zaidi call 0713155051
   
Loading...