Mwananchi wamepoteza umakini

Mwananchi wamepoteza umakini

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
950
Katika gazeti la leo tarehe 12.02.2013 issue Na.4614 Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mwananchi /Mchapisha amejihirisha kukosa umakini kwa kurudia habari hiyo hiyo moja ikiwa na vichwa vya habari na waandishi tofauti.

Katika habari ya kwanza iliyoandikwa na Vicky Kimaro inasomeka " Madeni yaziabisha Simba, Yanga" hii hailelezi lolote kuhusu madeni lakini ya pili imeandikwa na Michael Momburi na Doris Maliyaga inasoma "Wapinzani Simba wajifua kwa Siri" nayo inafanana na ya juu ikielezea rai ya kocha wa Simba Patrick Liewig kuomba sapoti kubwa ya mashabiki kuhusu kufungwa fungwa na sare mfululizo za timu hiyo. Inaonekana labda hakuna uhariri unaofanyika na hivi vyombo vya habari.
 
wadau, hivi Theophil Makunga bado ni mhariri mtendaji mkuu wa Mwananchi?
 
Kwa sisi tunaozeekea Newsroom, hayo makosa ni ya kawaida kabisa. Ingekuwa ajabu kama makosa hayo yangekuwa ndani ya kitabu kinachoandaliwa kwa miezi au miaka kadhaa. kwa kazi ya nusu siku (kazi ya gazeti) makosa ya aina hii uliyoitaja ni kama mpishi kuzidisha chumvi katika mboga siku moja moja!

manyerere
 
Kwa sisi tunaozeekea Newsroom, hayo makosa ni ya kawaida kabisa. Ingekuwa ajabu kama makosa hayo yangekuwa ndani ya kitabu kinachoandaliwa kwa miezi au miaka kadhaa. kwa kazi ya nusu siku (kazi ya gazeti) makosa ya aina hii uliyoitaja ni kama mpishi kuzidisha chumvi katika mboga siku moja moja!

manyerere
sijui kama utaeleweka kirahisi kamanda
 
sijui kama utaeleweka kirahisi kamanda

Kamanda unajua hawa watu lazima waelewe. Kazi ya gazeti ni ngumu sana, tofauti na wanavyodhani kwamba inaweza kufanywa na kumalizwa kwa usahihi kwa asilimia 100. Fikiria, kama wenzetu wanapasua kichwa badala ya mguu, na mguu badala ya kichwa, sisi ni nani hata tusiwe na makosa (japo si makubwa kama ya wenzetu) Au tunahukumiwa kwa sababu tunaweka ubaoni na kila wa kujua kusoma anatusoma? Hao ambao maandishi yao hawayaweki ubaoni ukiyaona mbona utapatwa na mpasuko wa roho?

manyerere
 
Back
Top Bottom