GE2025 Mwananchi: Hata aje Trump! Mama Samia atashinda

GE2025 Mwananchi: Hata aje Trump! Mama Samia atashinda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakazi wa Masasi Mjini wameonesha mshikamano na upendo wa kipekee kwa kujitokeza kwa wingi katika kibanda umiza katikati ya mji kufuatilia kampeni za mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Wananchi wa rika zote, wake kwa waume, vijana kwa wazee, wamemiminika katika eneo hilo wakiwa na hamu kubwa ya kusikiliza sera na maelekezo ya Dk. Samia kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga.

Kwa kawaida vibanda hivyo hutumika kuonesha mechi za mpira na filamu za hadhara, lakini safari hii kimegeuka kuwa kivutio kikubwa cha kisiasa. Wamiliki wake wamesema idadi ya watu wanaokusanyika imeongezeka mara dufu tangu kampeni za CCM zianze rasmi.

Miongoni mwa waliokusanyika, mkazi mmoja amesema kwa mzaha: “Hata aje Donald Trump agombee na Samia, Samia atashinda,” akionesha imani yake kubwa kwa mgombea huyo. Akaongeza kwa utani kuwa baiskeli walizopewa mabalozi wa CCM zimekuwa na faida kubwa kwenye maisha yake binafsi, akidai zimemsaidia hata ‘kupata mke wa pili’ kauli iliyowafanya waliomsikiliza kulipuka kwa kicheko.

Wananchi wengi wameeleza kuvutiwa na namna Dk. Samia anavyowasilisha hoja zake kwa upole na hekima, huku akigusa moja kwa moja mahitaji ya wananchi wa kawaida kuhusu maendeleo ya wanawake, vijana, miundombinu na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

 
Trump anayumba! Siyo wa kumtegemea. Nani alidhani baada ya Kikao cha Alaska na Putin bado Jana angeandika maneno Yale ya kuwa Ukraine atakomboa maeneo yote na kisha kuivamia Russia!?
 
Huko Tanzania kuna habari gani? Huku USA tunaendelea na majukumu yetu ya kila siku , wasalime huko 🇹🇿
 
Back
Top Bottom