Mwananchi anapobeba laana ya watawala

Mwananchi anapobeba laana ya watawala

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
8,043
Reaction score
18,482
Ukimsaidia mtu yeyote, taasisi, kampuni au kikundi fulani kutenda uhalifu/uovu, nawe unakuwa mhalifu.

Raia mwema ni yule anayesaidia kuzuia kosa kutendeka.

Najaribu kutafakari mambo kadhaa:

1) Serikali hujiendesha kwa kodi za sisi wananchi.

2) Jeshi la Polisi na majeshi mengine yote, huendeshwa kwa kodi zetu sisi wananchi

3) Magereza yanaendeshwa kwa kodi zetu wananchi.

4) Mahakama na Bunge vinaendeshwa kwa kodi zetu wananchi.

5) Halikadhalika ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali, DPP, TAKUKURU, TISS, na TRA.

Matukio ya siku za karibuni na yanayoendelea:

1) Serikali kwa kutumia ofisi ya DPP, TAKUKURU, TRA, TISS, Polisi wanatumika kuwabambikia watu kesi za ugaidi, uhujumu uchumi, madawa ya kulevya, utakatishaji fedha, n.k. Kubambikia watu kesi ni uovu. Na wananchi tumeshiriki katika uovu huu kwa sababu hawa wote wanawezeshwa kutenda uharamia huo kwa kutumia kodi zetu.

2) Wasiojulikana wanaojulikana wametumika kuteka watu, kuua, kuwapoteza na kuwatesa watu. Hawa wanayakamilisha hayo kutokana na kodi zetu, indirectly tumeshiriki katika huo uharamia kwa sababu tuliwawezesha kifedha.

3) Bunge limetumika kupitisha sheria haramia dhidi ya wananchi ikiwemo sheria zinazoondoa uhuru wa maoni, kodi dhulumati, kuwafukuza wawakilishi wa wananvlchi wakati vikao vikiendelea. Tumeliwezesha Bunge kufanya huu uharamia kwa kodi zetu.

4) Mahakama, kwa uwazi kabisa imetumika kuwatesa watu ambao wanaikosoa serikali, maDC, maRC, mara kadhaa wametumika kuwaumiza wananchi walipa kodi.

KWA NAMNA GANI TUTAIKWEPA HUKUMU KWA UOVU WETU:

1) Tunavifadhili vyombo vya serikali kufanya uharamia.

2) Tunalifadhili Bunge kutunga sheria za kidikteta zinazotutesa sisi na watoto wetu ambao hawana uwezo wa kuzuia.

3) Tunaifadhili ofisi ya DPP kuwaandalia kesi za kuwabambikia kesi ndugu zetu.

4) Tunaifadhili mahakama ili iwafunge ndugu zetu wasio na hatia

Kwa kushiriki huu uovu kwa ukamilifu au kwa kiwango fulani, tunatenganishwa vipi na waovu? Tunafanya nini kusaidia kuzuia uovu? Tusiseme hatuna uwezo au namna, kila mmoja ana uwezo wa kiwango fulani katika kuzuia uovu kutendeka kwa kadiri alivyojaliwa na Mungu.

Tafakari yangu ya Jumapili hii - nifanye nini ili nisihebike pamoja na waovu. Roho wa Mungu atuongoze.
 
Huu ufadhili uliouzungumzia hapa unafanywa na wananchi bila wao kupenda, hao TRA wakienda kuchukua kodi kwenye ofisi yangu serikali ndio inayoamua matumizi ya hiyo kodi, sio mimi, na hivyo hiyo kodi ndio inatumika kuwalipa mishahara polisi wanaowaonea wapinzani.

Naamini better solutiona ya hiki ulichokiandika hapa ni Katiba Mpya, Katiba itakayoainisha majukumu na mipaka ya watawala wa serikali na kipi kitakachowapata (adhabu) pale wakienda kinyume na utekelezaji wa majukumu yao.

Hii itasaidia kuelekeza kinachokusanywa na serikali kutumika kwa njia halali bila kuonea kikundi fulani cha watu (wapinzani), hivyo kutuepusha wananchi na hiyo dhambi uliyoandika hapo juu.
 
Polisi iwe idara ndani ya JWTZ.
Na IGP ateuliwe na kamati maalumu chini ya usimamizi wa CDF.
 
Mimi naamini kuna siku inakuja wote hatutaamini kitakachotokea kamwe

IMG_20210808_100228.jpg
 
Dunia inaendeshwa na akili ya wastani, au watu wa wastani katika jamii. Hitler alifanya aliyofanya kwa sababu watu wa wastani Ujerumani waliunga mkono fikra zake. Naambie kuhusu uelewa wa Mtanzania wa wastani kwa sasa. Kisha peleka mashtaka kwa sala kwa Mwenyezi Mungu utakapokuwa Kanisani. Jumapili njema.
 
Kama serikali inabambikia watu kesi... Je wakati Sabaya anabambikiwa kesi Mbowe na viongozi wengine wa kisiasa walifanyaje ili kuhakikisha hali hiyo haiendelei kutokea?
 
Kama serikali inabambikia watu kesi... Je wakati Sabaya anabambikiwa kesi Mbowe na viongozi wengine wa kisiasa walifanyaje ili kuhakikisha hali hiyo haiendelei kutokea?
7ya alituhumiwa na jamii kipindi chote cha mamlaka yake.
 
Kama serikali inabambikia watu kesi... Je wakati Sabaya anabambikiwa kesi Mbowe na viongozi wengine wa kisiasa walifanyaje ili kuhakikisha hali hiyo haiendelei kutokea?
Kesi ya Sabaya ni tofauti sana na ya Mbowe. Sabaya analalamikiwa na wananchi wengi kwenye eneo alilokuwa akiishi na kule alikokuwa anafanyia kazi.

Kwa Mbowe, walalamikaji ni Jeshi la Polisi ambalo sifa yake kubwa ni kuwaonea raia kwa kuwabambikia kesi wananchi.

Kitu kimoja kilicho dhahiri ni kwamba hatuna mahakama ambayo ni mahakama katika tafsiri inayotakiwa. Hivyo Mbowe na Sabaya, watatendewa namna ambavyo watawala wanataka na siyo kwa kuzingatia haki.
 
Back
Top Bottom