Mwanamuzi"Sean Kingston"apata ajali mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamuzi"Sean Kingston"apata ajali mbaya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjunguonline, Jun 1, 2011.

 1. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamuziki machachari katika sekta ya Raga, Sean Kingston wa Jamaica, ambaye alipata ajali mbaya siku ya Jumapili, anaripotiwa kuwa anaendelea vizuri.

  Kingston alipata ajali hiyo akiendesha pikipiki ya kwenye maji, Jet Ski, katika ufukwe wa bahari huko Miami, Florida. Kingston alikuwa akiendesha pikipiki hiyo ya mwendo kasi huku akiwa amepakia abiria wa kike, majira ya jioni ya Jumapili.
  Inasemekana Kingston alishindwa kukimiliki vyema chombo hicho na hatimae kwenda kujibamiza katika ukingo wa daraja. Kingston na abiria wake waliokolewa na boti moja ndogo iliyokuwa ikipita karibu yao na baadae kuwahishwa hospitali na kikosi cha zima moyo cha Miami.

  Awali, hospitali ya Jackson Memorial ilitoa taarifa kwamba mwanamuziki huyo alikuwa hoi bin taaban, lakini sasa habari zinasema kwamba jamaa anajitambua.

  Abiria wa Kingstona yuko buheri wa afya na anaisaidia polisi kwa uchunguzi, kwa mujibu wa wavuti ya Local10. com

  Kingston alianza kuwika katika tasnia ya muziki mapema 2007 akiwa na singo yake ya Beautiful Girls.

  Singo hiyo ilikamata
  chati za nchini Marekani na Uingereza. Ameshafayatua vibao vingine matata akishirikiana na wakali kama Justin Bieber na Natasha Bedingfield. Albamu yake ya tatu inategemewa kuachiwa baadae mwaka huu.

  http://www.guardian.co. uk/music/2011/may/31/ sean-kingston-jet-ski-c...
   
Loading...