The Certified
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 910
- 773
(Upasuaji huo ulichukua saa 56 na ulishirikisha madaktari 60)
Tarehe 16 mwezi Juni 2016 Andy Sandness alisafirishwa na kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji katika kliniki ya Mayo huko Rochester Minnesota ili kufanyiwa upasuaji usio wa kawaida duniani.
Wiki tatu baadaye alijiangalia kwenye kioo asijue ni nini angeona.
Sura alioona katika kioo haikuwa yake bali ya mtu mwengine ,pua, mashavu, mdomo, taya kidevu na hata meno ya mtu aliyemfadhili kiungo hicho Calen Ross.
Kile watu hao wawili waliokuwa nacho ambacho kilikuwa kikifanana wakiwa na umri wa miaka 21 walijishikia bunduki.
Akishindwa kuzungumza vizuri baada ya kuona uso wake mpya ,bwana Sandness aliandika ujumbe kwa madaktari wake na familia akisema.'Sikutarajia'' .
Bwana Sandness kutoka eneo la Wyoming aliwachwa na uso uliokuwa umeharibiwa kabisa baada ya jaribio la kujiua 2006.
Baada ya kufanyiwa upasuaji aliwaambia watu kumwelezea vile alivyo.
Bwana Ross ambaye aliishi Minnesota hakupona alipojipiga risasi mwaka 2016 na kumwacha nyuma mjane aliyekuwa na mimba Lily asijue la kufanya.
Alitaka kutekeleza wazo la mumewe la kufadhili viungo lakini aliogopa mtu mwengine kuchukua uso wake.
Sikutaka nitembee halafu kwa bahati nimuone Calen, aliambia chombo cha habari cha Ap.
Lakini alikubali baada ya kuhakikishiwa kwamba bwana Sandness alikuwa na macho na paji lake la uso na hatofanana na marehemu mumewe.
Daktari Samir Mardani mtaalam wa utengezaji wa uso alitumia zaidi ya miaka mitatu akijifunza upasuaji na upandikizaji wa nyuso za vichwa vya maiti.
Walikadiria kwamba itachukua miaka kadhaa kupata mfadhili wa uso wake, lakini miezi mitano baada ya Sandness kuwekwa katika orodha ya kusubiri mfadhili wa uso alipata uso wa bwana Calen.
Upasuaji na upandikizaji huo mgumu ulishirikisha kushikanisha mishipa sawa katika nyuso zote mbili na kutumia umeme kubaini majukumu yao kwa mfano mtu anapotabasamu, kufunga na kufungua na kufunga macho.
Ilikuwa muhimu kwa bwana Sandness kufanya vitu kwa kutumia uso wake mpya.
Bwana Sandness mwenye umri wa miaka 31 na Lily hawajaonana.
Lakini amemuandikia barua, ambapo alizungumzia kuhusu vitu alivyopenda mumewe.
''Ataendelea kupenda uwindaji na uvuvi na mbwa kupitia mimi',aliandika