Mwanamume anayeshutumiwa kwa kumshambulia Rais wa Mali afariki dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
Mwanamume anayetuhumiwa kujaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali, Assimi Goïta, wiki iliyopita amekufa hospitalini akiwa chini ya ulinzi, serikali inasema.

Mshambuliaji huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio lake, ambalo lilifanyika wakati Bwana Goïta akihudhuria sala katika msikiti.

Taarifa ya serikali ilisema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini, ambako alikufa.Sababu ya kifo chake inachunguzwa .Bwana Goïta ameongoza mapinduzi mawili nchini Mali katika mwaka uliopita.

1627290079624.gif
 
Africans bado tuna safari ndefu sana, kuna mawili, moja kifo kimesababishwa na kichapo heavy kutoka kwa walinzi na pili yawezekana waliotaka kumuua raisi wapo ndani ya system so wameamua kumuua ili siri ibakie siri. Lakini pia kama raisi aliingia madarakani kwa kupundua wenzake unadhani yeye atatoka madarakani kwa njia gani? Kupinduliwa au kuuawa, pens down!!!!
 
Back
Top Bottom