Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267

Akiongea na wanahabari kituo cha polisi cha Maua anakozuiliwa, Julias Rigo Mwithali kutoka Kangeta kaunti ndogo ya Igembe Kati, alisema yeye ni mfuasi sugu wa Bw Odinga na alining'inia katika helikopta yake ili ampeleke nyumbani kwake na ampe kazi

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye aliachia masomo yake katika darasa la nne alisema aliruka kutoka katika helikopta hiyo katika shule ya msingi ya Athimba, Igembe Kusini na kuchukua boda boda kurudi nyumbani
Kamanda wa polisi Meru, Bw Nelson Taliti alithibitisha kukamatwa kwa Bw Rigo, baada ya safari hiyo ya hatari, Bw Taliti alieleza kuwa Mwanamume huyo alishukishwa katika shule ya msingi ya Athimba baada ya Rubani kutua ghafla
Mwanamume huyo alishuka akiwa salama bila majeraha yoyote baada ya kusafiri kwa zaidi ya kilometa 15 kutoka uwanja wa Maili Tatu ambapo helikopta hiyo ilipaa
Bw. Odinga alikuwa amezuru eneo hilo kuhimiza watu wajitokeze kusajiliwa kama wapiga kura
Rubani aliposikia nduru kutoka kwa umati wa watu alijaribu kwenda taratibu ili ampatie nafasi ya kushuka lakini Mwanamume huyo aliendelea kushikilia helikopta huku akiwapungia watu mkono
Wakazi walisema Bw Rigo alikuwa ameapa kuandamana na Bw Odinga hadi Nairobi kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kupata nafasi ya kupanda helikopta
"Alikuwa akisema anataka kupanda helikopta kwa mara ya kwanza na kwamba lazima iwe ya Raila Odinga", alieleza mkazi Bw John Mwiti
Wenyeji waliwashtumu polisi kwa kuzembea kazini wakisema kuwa Mwanamume huyo angeweza kuzuiwa kupanda ikiwa maafisa wangekuwa macho
Mwaka 2016, Saleh Wanjala ambaye alikuja kufahamika maarufu kama 'James Bond wa Bungoma' alining'inia kwenye helikopta iliyokuwa imeubeba mwili wa Mfanyabiashara aliyeuawa Jacob Juma katika Kaunti ya Bungoma. Alishtakiwa kwa kuhatarisha maisha yake.