Afisa wa Polisi akamatwa kwa kurusha bomu la machozi ndani ya 'guest' baada ya kumfumania mpenzie na mwanaume mwengine

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Polisi mjini Kisumu wanamshikilia mwenzao baada ya kurusha vitoa machozi ndani ya 'guest' alimokuwa mpenzie akila uroda na mwanaume mwengine.

Tukio hilo lilitokea eneo la Nyamasaria kaunti ya Kisumu mwendo wa saa alfajiri.

Juhudi za wafanyakazi wa 'guest' kumzuia askari Polisi huyo kutoingia humo hazikufua dafu na ndipo aliamua kufyatua mabomu kadhaa ya machozi.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kisumu Mashariki Joseph Asugo amesema kuwa polisi wamefungua jalada la uchunguzi na watamfungulia mashataka kwa matumizi mabaya ya vitoa machozi.

Kwa sasa Afisa huyo kutoka kituo cha polisi cha Kasagam anapokea matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wakiburudika ndani ya baa iliyoko mkabala na eneo la tukio
 
Back
Top Bottom